Tabia ya Wafanyakazi wa Shirika la Umeme kujiungia Umeme bila ya kufuata utaratibu na Sheria zilizowekwa kumesababaisha baadhi ya Wafanyakazi wa shirika hilo kusimamishwa kazi kwa kupitisha uchunguzi.
Akizungumza na Wafanyakazi wa Shirika hilo Waziri wa Maji, Nishati na Madini Mhe Shaibu Hassan Kaduara amesema kutokana na kukiuka Sheria na maadili ya kazi Shirika hilo halitomvumilia Mfanyakazi yoyote atakae bainika kuliibia Shirika ilo.
Kauli iyo ameitoa baada ya kuwasimamisha kazi Wafanyazi Kumi na Tano wa Shirika la umeme baada ya kubainika na makosa ya kujiungia Umeme kinyume na Sheria.
Meneja Mkuu wa Shirika la Umeme Zanzibar Haji Haji amesema kiwango kikubwa cha utaalamu ndicho kinachotumika katika kuibia Umeme ambacho kiwango hicho kinafanywa na Mfanyakazi wa Shirika na si Mtu Binafsi ambae itia hasara Serikali na kuikoseha pato la Taifa