SMZ YAJIPANGA KULETA MAGEUZI SEKTA YA KILIMO

Dkt.Mwinyi

      Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dkt.Hussein Ali Mwinyi amesema Serikali imedhamiria kuleta mageuzi ya kilimo nchini kwa kukifanya kilimo biashara chenye tija kwa kuimarisha mnyororo wa thamani kutoka shambani hadi kwa mlaji.

     Dkt.Mwinyi aliyasema hayo tarehe 3 Julai 2024 alipofungua maonesho ya saba ya kilimo ya Nane Nane Zanzibar katika viwanja vya Dole , Kizimbani Mkoa wa Mjini.

      Aidha Rais Dkt.Mwinyi amesema Serikali itaanzisha vituo maalum kila wilaya kuhamasisha upatikanaji wa huduma kwa wakulima na wafugaji nchini.

     Halikadhalika Rais Dkt.Mwinyi ameleeza kuwa Serikali inatarajia kutekeleza mradi mkubwa wa mageuzi wa uzalishaji wa wafugaji wa maziwa kwa wafugaji wadogo wadogo ambao utazingatia mabadiliko ya tabia nchi yenye gharama za shilingi bilioni 7.5.

     Rais Dkt.Mwinyi ametoa wito kwa vijana kutumia fursa zilizopo katika sekta ya kilimo na mifugo kwa kujiajiri , pia amewahimiza wajifunze mbinu bora za kilimo na ufugaji kupitia maonesho ya kilimo.

stories
standard
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.