RAIS SAMIA AMEIAGIZA WIZARA YA AFYA KUKAMILILISHA UTAFITI WA KITAIFA

RAIS WA JAMUHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan ameiagiza Wizara ya Afya kukamililisha utafiti wa Kitaifa utakaobainisha hali halisi ya Wataalamu wa Afya Nchini waliopo kwenye Soko la Ajira, mahitaji na namna bora itakayoiwezesha serikali kutatua tatizo la kuajiri katika sekta hiyo.

Raisi Dr. Samia ametoa maagizo hayo katika kilele cha kumbukizi ya Tatu ya Hayati Benjamin William Mkapa iliyofanyika Jijini Dar Es Salam na kuhudhuriwa na Viongozi mbalimbali ambapo pia ameitaka wizara ya mambo ya Nje na ushirikiano wa Afrika mashariki kutengeneza Mkakati wa Diplomasia ya Afya na kusaidia upatikanaji wa nafasi za Mafunzo ya juu kwa wataalamu wa Sekta ya Afya.

Amesema kuwa suala la ajira za Sekta ya Afya linaendana na kukua kwa Uchumi, na halina matokeo ya haraka hivyo amesisitiza juu ya umuhimu wa kuchapa kazi kwa bidii na umuhimu wa kufanya kazi kwa pamoja katika kufikia mafanikio ya Sekta hiyo. 

Aidha, Dr Samia amewataka Wataalamu wa Afya wa pande Mbili za Muungano kubadilishana uzoefu na kujadili kwa pamoja changamoto za Afya tulizonazo namna bora ya kuzitatua kwa pamoja.

Kwa upande wake Waziri wa Afya Ummi Mwalimu amemueleza Raisi Samia maadhimio yaliyofikiwa katika Mkutano wa Siku Mbili uliojadili rasilimali Watu katika Sekta afya.

Kongamano la Tatu la Kumkumbuka Hayati Benjamin Mkapa limefanyika kwa siku Tatu Jijini Dar Es Salaam likiwa na lengo la kuenzi maono na mchango wake alioutoa kwa TAIFA la Tanzania.             

stories
standard
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.