Waziri wa Nchi Ofisi ya Raisi Fedha na Mipango Dkt.Sada Mkuya Salum amewataka Wafanyakazi wa Wizara hiyo na Taasisi zilizopo chini yake kuhakikisha wanatekeleza mipango kazi iliyopitishwa katika Mkutano Mkuu wa Bodi ya Wafanyakazi.
Akizungumza na Wafanyakazi hao katika Mkutano wa Mwaka Mpya wa Fedha na Bodi ya Wafanyakazi wa Wizara ya Fedha na Mipango na Taasisi zilizopo chini ya Wizara hiyo Mhe.Sada amesema lengo la Mkutano ni kupanga utekelezaji mpya wa Mwaka wa Fedha ili kutoa huduma bora kwa Wananchi.
Amesema kupitia Mkutano huo kumechangia Maendeleo makubwa katika Sekta za Umma hasa kupitia Taasisi za Fedha na kufanikisha Miradi mikubwa ya maendeleo Nchini ikiwemo Barabara na Masoko.
Akitoa mafanikio ya maadhimio ya Mkutano wa Mwaka Mpya wa Fedha 2023 2024 Mkurugenzi wa Uendeshaji na Utumishi Wizara ya Fedha na Mipango Ndg.Rajab Yakoub amesema kupitia maadhimio yaliyotolewa katika Kikao hicho wameweza kutekeleza mipango mbalimbali ikiwemo kuwazingatia Watu Wenye Mahitaji Maalum katika huduma za Fedha lugha nzuri za Viongozi kwa Wafanyakazi wao pamoja na mabadiliko ya Mishahara kwa Wahasibu.