MECCO IMEHIMIZWA KUKAMILISHA UJENZI BARABARA YA CHAKE-WETE

MAKAMO WA PILI WA RAIS ZANZIBAR

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla amemuhimiza Mkandarasi wa kampuni ya Ujenzi ya Mecco inayojenga barabara ya Chake-Wete, kufanya uharaka wa kukamilisha Ujenzi wa Barabara hiyo ili kujenga imani ya Wananchi na kuwaondolea usumbufu.

Makamu wa pili wa Rais akiwa katika ziara ya kukagua Maendeleo ya Ujenzi wa Miradi mbali mbali ya maendeleo ikiwemo Barabara ya Chake-Wete ambayo inatarajiwa ikamilike mwishoni mwa Mwezi wa Nane Mwaka huu, amesema kutokamalika kwa wakati kutaleta shida kwa Wananchi wanaotumia Barabara hiyo kwa shughuli za kujitatafutia kipato.

Amesema ni vyema Wakandarasi wakahakikisha wanatimiza makubaliano ya Mikataba ili kuepuka hasara kwa Serikali.

Katika hatua nyengine ya ukaguzi wa Ujenzi wa Soko la Samaki na Mboga Mboga lililopo Mzambarau takao na Soko la Wajasiri Amali kifumbikai Wete, Makamu wa Pili wa Rais ametoa Mwezi mmoja kwa Wananchi waliokwisha kulipwa fidia kuondoka katika eneo hilo ili kupisha Ujenzi wa soko pamoja na utanuzi wa Barabara, huku akiahidi Serikali itaendelea kutoa ushirikiano kwa Kampuni zinazojenga Miradi ya maendeleo Zanzibar ili kuhakikisha inamalizika kwa wakati uliopangwa na kuwaondolea Kero Wananchi.

Kwa upande wao Mawaziri wa Wizara zenye dhamana ya kusimamia Miradi hio wamesema kuwa watahakikisha kwa hali yoyote ile Miradi inamalizika kwa wakati uliopangwa ili kuendana na Dhamira ya Serikali ya kuwaletea maendeleo Wananchi wake.

Wakandarasi wanaojenga Miradi hiyo wamesema ujio wa Mhe. Makamu wa Pili wa Rais utatatua matatizo mbali mbali yanayowakabili ikiwa ni pamoja na kucheleweshewa malipo jambo ambalo husababisha kuzorota kwa ujenzi wa Miradi.

Miradi mengine iliyokaguliwa ni Soko la wajasiriamali Kifumbikai, Ujenzi wa Kituo cha afya Jadida, Ujenzi wa Nyumba za Madaktari Kinyasini, kukaguua maendeleo ya Hospital ya Wilaya Kinyasini.

stories
standard
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.