HOFU YAWAJAA WAKAAZI WA KARAKARA KUTOKANA NA JAA LILOPO KATIKA ENEO LAO

TAKA KARAKANA

    Kuwepo Jaa kubwa katika Eneo la Karakana ambalo ni Makaazi ya Watu pamoja Wafanyabiashara, limetajwa kuwa Tishio na usalama wa Afya zao.

    Jaa hilo ambalo kwa mujibu wa Wafanyabiashara wa Eneo hilo, wamesema linakadiriwa kuwepo kwa Miezi Mitatu bila ya kuchukuliwa Taka hizo, linaleta hofu kutokana na harufu inayosambaa pamoja na Wadudu na kukwamisha Biashara.

     ZBC ikazungumza na Naibu Sheha Shehia ya Karakana Kadir Khatib Hamad, amesema Uongozi wa Shehia Umeripoti kuwepo taka nyingi katika Jaa hilo, lakini hadi sasa hakuna utekelezaji wowote.

    Kwa upande wa athari za Kiafya kutokana na Jaa hilo, msimamizi Mkuu wa Taka kutoka Wizara ya Afya Rahim Shehe Makame, anaelezea hatari zinazoweza kusababishwa na Taka hizo.

     Akizungumzia Jaa hilo Afisa Mazingira Manispaa ya Mjini ambayo ndiyo yenye dhamana ya kusimamia Majaa, Ndg.Mohamed Kassim Suleiman, amesema awali walilifunga Jaa hilo lakini inaonekana Wananchi wamekaidi hatua hiyo.

    Inatajwa kuwa kuna uzalishaji Mkubwa wa Taka za Majumbani katika Wilaya ya Mjini ambazo haziendani na uwepo wa Majaa yaliyopo.

stories
standard
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.