Waziri wa Nchi, Afisi ya Rais, Fedha na Mipango Dk. Saada Mkuya Salum amesema Serikali imetayarisha huduma za Bima kwa wageni wanaoingia Zanzibar inayotarajia kuanza septemba mwaka huu.
Akizungumza na Wadau wa usafiri wa Mashirika ya Ndege ya Nje na ndani ya Nchi amesema Taratibu zinaendelea kukamilika na Bima hiyo itasisha huduma za Afya na nyingine wakati wote anapokuwa Nchini.
Amesema Serikali inaendelea kuimarisha huduma za Afya na Miundombinu ya Kiuchumi ili kuona Zanzibar inakuwa sehemu Nzuri ya kufikia Wageni.
Nae Kaimu Mkurugenzi Mwendeshaji wa Shirika la Bima Zanzibar Ussi Jape Khamis amesema kuanzishwa bima hiyo itawavutia wageni wanaoingia nchini wakiwemo Wawatalii.
Amesema Bima hiyo pia itahusisha upotevu Mizigo, Maradhi au kufarikidunia ili kupatiwa huduma za haraka