MABARAZA YA MANISPAA KUWAONDOA WAFANYA BIASHARA NA WAENDESHA BODA BODA SEHEMU ZISIZO RASMI

RC KITWANA

Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharib Idrisa Kitwana Mustafa ametoa muda wa Siku Tatu kwa Mabaraza ya Manispaa ndani ya Mkoa huo kuwaondoa Wafanya Biashara na waendesha Boda Boda kwenye maeneo yasio rasmi ya Watembea kwa Miguu ili kuhakikisha Mji unakuwa na haiba nzuri.

Agizo hilo amelitoa wakati akizungumza na  Vyombo vya habari kuhusiana na Operesheni huo amesema ni marufuku kuendesha Gari na Vyombo vya moto vyengine   katika    Njia za watembea kwa miguu ili kupunguza Ajali za Barabarani zinazojitokeza mara kwa mara .

Amesema Serikali imekuwa ikitumia Fedha nyingi ili  kuhakikisha  wanaimarisha Miundo Mbinu  ya kisasa katika kuleta maendeleo mbali mbali  ili kuweza  kudumisha hali ya usafi katika maeneo yote ya Zanzibar  .

Aidha Mkuu wa Mkoa amesema katika kuhakikisha hali ya usafi wa mazingira inaimarika katika maeneo yote ni vyema Baraza   la Manispaa kulitilia mkazo suala hilo kwa kuwachukulia hatua watao kiuka Sheria  zilizowekwa pamoja  Mabaraza yatakayofanya vibaya .

Tags
stories
standard
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.