Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharib Idrisa Kitwana Mustafa ametoa muda wa Siku Tatu kwa Mabaraza ya Manispaa ndani ya Mkoa huo kuwaondoa Wafanya Biashara na waendesha Boda Boda kwenye maeneo yasio rasmi ya Watembea kwa Miguu ili kuhakikisha Mji unakuwa na haiba nzuri.
Agizo hilo amelitoa wakati akizungumza na Vyombo vya habari kuhusiana na Operesheni huo amesema ni marufuku kuendesha Gari na Vyombo vya moto vyengine katika Njia za watembea kwa miguu ili kupunguza Ajali za Barabarani zinazojitokeza mara kwa mara .
Amesema Serikali imekuwa ikitumia Fedha nyingi ili kuhakikisha wanaimarisha Miundo Mbinu ya kisasa katika kuleta maendeleo mbali mbali ili kuweza kudumisha hali ya usafi katika maeneo yote ya Zanzibar .
Aidha Mkuu wa Mkoa amesema katika kuhakikisha hali ya usafi wa mazingira inaimarika katika maeneo yote ni vyema Baraza la Manispaa kulitilia mkazo suala hilo kwa kuwachukulia hatua watao kiuka Sheria zilizowekwa pamoja Mabaraza yatakayofanya vibaya .