Rais Wa Zanzibar Na Mwenyekiti Wa Baraza La Mapinduzi Alhaj Dkt. Hussein Ali Mwinyi Amewataka Wananchi Kuhakikisha Wanaitumia Misikiti Kwa Kufanya Ibada Na Taaluma Nyingine Ili Kuleta Maslahi Mapana Kwa Ujenzi Wa Maisha Ya Dunia Na Akhera.
Dk Mwinyi Ameyasema Hayo Katika Hafla Ya Ufunguzi Wa Msikiti Wa Ijumaa Chachani Wilaya Ya Chake Mkoa Wa Kusini Pemba.
Alhaj Doctor Mwinyi Amesema Misikiti Ni Mahapa Pekee Pa Kukutana Na Kujadili Masuala Yanayoikabili Jamii Ikiwemo Kuwa Saidia Mayatima Wajane Na Wasiojiweza Il Kujenga Mustakbali Mwema Wa Maisha Na Mendeleo Yao
Awali Mjenzi Wa Msikiti Huo Shkh Said Nassor Bopar Mbali Na Ujenzi Huo Amemuomba Rais Kumuandalia Meli Ambayo Itachukua Mizigo Ya
Wafanyabiashara Ikiwemo Safari Za Swadaqa Za Ramadan Kutokana Na Zilizopo Kushindwa Kukidhi Shida Ya Upatikanaji Wa Haraka Wa Chakula Kwa Wananchi Wa Pemba.
Katika Risala Iliyosomwa Na Ustadhi Ali Abdalla Nassor Amesema Katika Kuweka Mazingira Bora Ya Ibada Na Taaluma Msikiti Huo Unahitaji Madrasa Itakayokuza Maadili Mema Ya Usimamizi Wa Msikiti
Kwa Vijana , Viongozi Na Waumini Wao.
Naye Naibu Muft Kwa Niaba Ya Mufti Mkuu Wa Zanzibar Sheikh Mahmoud Mussa Wadi Amewataka Viongozi Wa Msikiti Wa Chachani Kuwa Na Subira Katika Mambo Yanayorudisha Nyuma Utendaji Wa Shughuli Za Msikiti Huo Na Kwamba Kila Hatua Wazielekeze Kwa Ofisi Yake Kutafutiwa Suluhu.
