Jeshi la Polisi Mkoani Lindi inamshikilia mwanaume mmoja Hassan Athuman Mpogo (46) mwislam na mmwera mkazi wa Somanga Wilayani Kilwa Mkoani Lindi kwa tuhuma za kumuua aliekuwa mke wake kwa kumkata na panga Katika sehemu mbali mbali za mwili wake
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Lindi, ACP John Imori, amesema tukio Hilo kimetokea April 26, 2026 ambapo mtuhumiwa alimshambulia mwanamke huyo na kumjeruhi sehemu mbalimbali za mwili, hali iliyosababisha kifo chake alipokuwa akipelekwa kituo cha afya.
Kwa mujibu wa ACP Imori, kabla ya tukio hilo mtuhumiwa alidai kushauriwa na mganga wa jadi, Haji Said Nguvunze (46), akiaminishwa kuwa angepona tatizo la nguvu za kiume ikiwa atamuua mke wake aliyemshuku kumroga.
Kamanda Imori ametoa wito kwa wananchi kuachana na imani za kishirikina na badala yake kutafuta huduma sahihi za afya wanapokumbwa na matatizo ya kiafya.
