ZRCP ELIMISHENI UMUHIMU WA MATOKEO YA TAFITI

Rais Wa Zanzibar Na Mwenyekiti Wa Baraza La Mapinduzi Dkt. Hussein Ali Mwinyi, Ameushauri Uongozi Wa Kituo Cha Tafiti Za Kiuchumi, Kijamii Na Uchambuzi Wa Sera Zanzibar –Zrcp- Kuandaa Mikutano Na Mijadala Na Wadau Ili Kuwaelimisha Kuhusu Umuhimu Wa Kutumia Matokeo Ya Tafiti Katika Utekelezaji Wa Majukumu Yao.

Ni Ziara Ya Ujumbe Wa Kituo Cha Tafiti Za Kiuchumi, Kijamii Na Uchambuzi Wa Sera Zanzibar –Zrcp- Katika Ikulu Ya Vuga Hapa Zanzibar.

TAASISI ZA UMMA ZATAKIWA KUZINGATIA UPENDO NA UADILIFU

Rais Wa Zanzibar Na Mwenyekiti Wa Baraza La Mapinduzi Dkt, Hussein Ali

Mwinyi Amewasisitiza Viongozi Wakuu Katika Taasisi Za Umma Kuzingatia Upendo,Uadilifu Na Haki Katika Kuwasimamia Wanaowaongoza Na Utekelezaji Wa Majukumu Yao. 

Akizungumza Katika Kongamano La Tatu La Kiimani Kwa Viongozi Wa Serikali Lililoandaliwa Na Afisi Ya Mufti Mkuu Wa Zanzibar, Ameeleza Kuwa Kongamano Hilo Ni Msingi Wa Kukumbushana Umuhimu Wa Kuzingatia Maadili Katika Utumishi Wa Umma Na Jukwaa Muhimu La Kujifunza Uwiano Wa Kazi Kwa Misingi Ya Kiimani 

DKT. MWINYI ATAKA MISIKITI ITUMIKE KWA MANUFAA YA DUNIA NA AKHERA

Rais Wa Zanzibar Na Mwenyekiti Wa Baraza La Mapinduzi Alhaj Dkt. Hussein Ali Mwinyi Amewataka Wananchi Kuhakikisha Wanaitumia Misikiti Kwa Kufanya Ibada Na Taaluma Nyingine Ili Kuleta Maslahi Mapana Kwa Ujenzi Wa Maisha Ya Dunia Na Akhera.

Dk Mwinyi Ameyasema Hayo Katika Hafla Ya Ufunguzi Wa Msikiti Wa Ijumaa Chachani Wilaya Ya Chake Mkoa Wa Kusini Pemba.

Alhaj Doctor Mwinyi Amesema Misikiti Ni Mahapa Pekee Pa Kukutana Na Kujadili Masuala Yanayoikabili Jamii Ikiwemo Kuwa Saidia Mayatima Wajane Na Wasiojiweza Il Kujenga Mustakbali Mwema Wa Maisha Na Mendeleo Yao

Subscribe to RAIS WA SERIKALI YA MAPINDUZI ZANZIBAR
 

Simplenews subscription

The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.