Makamu Wa Pili Wa Rais Wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla Amesema Msingi Mkubwa Ya Wiazara Ya Mambo Ya Ndani Ya Nchi Ni Kuhakikisha Inalinda Wananchi Na Mali Zao Pamoja Na Kutenda Haki Kwa Raia Wa Jamuhuri Ya Muungano Wa Tanzania.
Akizungumza Na Uongozi Wa Wizara Ya Mambo Ya Ndani Ya Nchi Uliofika Ofisini Kwake Baraza La Wawakilishi Chukwani Zanzibar Kwa Ajili Ya Kujitambulisha Amesema Suala La Usalama Wa Raia Na Mali Zao Ni Muhimu Katika Kuimarisha Nchi Kisiasa, Kiuchumi Na Kijamii
Mhe. Hemed Amevitaka Vyombo Vya Ulinzi Na Usalama Kutekeleza Majukumu Yao Kwa Kuzingatia Katiba , Sheria Na Miongozo Mbali Mmbali Ili Kuwa Na Utawala Bora Katika Kuwahudumia Wananchi Wa Jamuhuri Ya Muungano Wa Tanzaniawaziri Wa Wizara Ya Mambo Ya Ndani Ya Nchi Mhe. Patrobas Pascal Katambi Amesema Dhamana Waliyopewa Ya Kuhakikisha Ulinzi Na Usalama Wa Wananchi Na Mali Zao Ni Kubwa Hivyo Ameahidi Kufanya Kazi Kwa Kufuata Misingi Ya Kikatiba
Katika Ziara Hiyo Mhe. Katambi Ameambatana Na Mhe. Ayoub Mohammed Mahmoud Naibu Waziri Wa Mambo Ya Ndani Ally Senga Gugu Katibu Mkuu Na Miriyam Pereele Mmbanga Mkurugenzi Wa Diviseni Ya Utawala Na Usimamizi Wa Rasilimali Watu
