VYOMBO VYA ULINZI VIMETAKIWA KUTEKELEZA MAJUKUMU YAO KIKATIBA

Makamu Wa Pili Wa Rais Wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla Amesema Msingi Mkubwa Ya Wiazara Ya Mambo Ya Ndani Ya Nchi Ni Kuhakikisha Inalinda Wananchi Na Mali Zao Pamoja Na Kutenda Haki Kwa Raia Wa Jamuhuri Ya Muungano Wa Tanzania.

Akizungumza Na Uongozi Wa Wizara Ya Mambo Ya Ndani Ya Nchi Uliofika Ofisini Kwake Baraza La Wawakilishi Chukwani Zanzibar Kwa Ajili Ya Kujitambulisha Amesema Suala La Usalama Wa Raia Na Mali Zao Ni Muhimu  Katika Kuimarisha Nchi Kisiasa,  Kiuchumi Na Kijamii 

SMZ YAWEKEZA ZAIDI YA SH. BIL. 13 KATIKA MAHAKAMA

Serikali Ya Mapinduzi Ya Zanzibar Imechukua Hatua Thabiti Ya Kuweka Mazingira Bora Ya Kufanyia Kazi Kwa Mhimili Wa Mahakama.

Amesema Katika Mwaka Wa Fedha 2025/2026 Serikali Imewekeza Zaidi Ya Fedha Za Kitanzania Shilingi Bilioni 13.6 Kwa Ajili Ya Ujenzi Wa Majengo Ya Kisasa Ya Mahakama Ambayo Yanaendana Na Uwekaji Wa Miundombinu Ya Tehama.

Baada Ya Shamrashamra Ya Wiki Ya Sheria, Hatimae Kilele Cha Maadhimisho Hayo Yamefanyika Kisiwani Pemba.

MHE. HEMED ATIA SHIME UPATIKANAJI WA DAWA ZA KISUKARI

Makamu Wa Pili Wa Rais Wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla Amesema Serikali Inawajibu Wa Kuweka Mazingira Wezeshi Kupitia Sera Madhubuti, Ufadhili Endelevu Na Ushirikiano Utakao Hakikisha  Changamoto Kubwa Ya Ukosekanaji Wa Dawa Ya Insulini Kwa Watu Wanaoishi Na Ugonjwa Wa Kisukari Inapatiwa Ufumbuzi Wa Haraka.

Subscribe to MAKAMO WA PILI WA RAIS ZANZIBAR
 

Simplenews subscription

The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.