Makamu Wa Pili Wa Rais Wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla Amesema Serikali Inawajibu Wa Kuweka Mazingira Wezeshi Kupitia Sera Madhubuti, Ufadhili Endelevu Na Ushirikiano Utakao Hakikisha Changamoto Kubwa Ya Ukosekanaji Wa Dawa Ya Insulini Kwa Watu Wanaoishi Na Ugonjwa Wa Kisukari Inapatiwa Ufumbuzi Wa Haraka.
Mhe. Hemed Ameyasema Hayo Kwa Niaba Ya Rais Wa Zanzibar Na Mwenyekiti Wa Baraza La Mapinduzi Dkt Hussein Ali Mwinyi Katika Ufunguzi Wa Mkutano Wa Kimataifa Wa Kushughulikia Changamoto Na Vikwazo Vya Upatikanaji Na Usambazaji Wa Dawa Ya Insulini Unaofanyika Zanzibar.
Mhe.Hemed Amefahamisha Kuwa Jitihada Za Pamoja Za Kikanda Zinahitajika Ili K Upatikanaji Wa Dawa Ya Insulini Ufikie Malengo Ambapo Kwa Upande Wa Tanzania Juhudi Zinaelekezwa Katika Kinga, Uchunguzi Wa Mapema, Huduma Endelevu Pamoja Na Kuunga Mkono Utafiti Za Uzalishaji Wa Ndani Wa Dawa Za Insulini.
Kaimu Waziri Wa Afya Wa Zanzibar Dkt. Saada Mkuya Salum Amesema Mpango Wa Maendeleo Endelevu Wa Mwaka 2050 Umeweka Viashiria Muhimu Vya Utendaji Ambavyo Ni Pamoja Na Kupunguza Vifo Vinavyotokana Na Maradhi Yasiyo Ya Kuambukiza Kutoka Asilimia 4.9 Mwaka 2019 Hadi Asilimia 2.2 Itakapofika Mwaka 2050.
Kwa Upande Wake Dkt. Adelard Kakunze, Afisa Ufundi Mwandamizi Wa Magonjwa Yasiyo Ya Kuambukiza, Majeruhi Na Afya Ya Akili, Barani Afrika ( Cdc) Amesema Lengo La Mkutano Huo Ni Kujadili Kwa Pamoja Njia Sahihi Ya Kuhakikisha Dawa Ya Insulini Inapatikana Kwa Urahisi, Ubora Na Unafuu Kwa Ajili Ya Kuokoa Maisha Ya Watu Wengi Wanaoishi Na Ugonjwa Wa Kisukari.
