TEKNOLOJIA YA KILIMO KUMELETA MABADILIKO SEKTA YA KILIMO NA UFUGAJI.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman amesema kukuwa kwa matumizi ya teknolojia ya Kilimo nchini kumeleta mabadiliko makubwa katika Sekta ya Kilimo na UFugaji.

Amesema hayo wakati alipotembelea Maonesho ya Wakulima ya Nane Nane yanayoendelea katika Viwanja vya Dole kizimbani Wilaya ya Magharibi “A”. 

Amesema Maonesho yanatoa fursa kwa Wananchi kupata Taaluma ya kuweza kulima na kufuga kwa kutumia Mbinu za kisasa ambazo Mkulima huweza  kuvuna Mazao mengi kwa muda Mfupi.

HOSPITAL YA ABDALLA MZEE IMETAKIWA KUNUNUA MTAMBO MPYA WA KUCHOMEA TAKA

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla ameuagiza uongozi wa Hospitali ya Abdalla Mzee Mkoani Pemba kuhakikisha ndani ya kipindi cha Mwezi Mmoja wamenunua Mtambo mpya wa kuchomea Takataka za Hospitali ili kuepusha madhara.

Akikagua uendeshaji na utoaji wa huduma katika Hospitali hiyo amesema Uongozi unatakiwa kujipanga kuhakikisha huduma zote muhimu zinapatikana kwa wakati unaostahiki amesema kuwepo kwa Mtambo huo kutawasaidia Wafanyakazi kufanya kazi zao kwa ufanisi.

MECCO IMEHIMIZWA KUKAMILISHA UJENZI BARABARA YA CHAKE-WETE

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla amemuhimiza Mkandarasi wa kampuni ya Ujenzi ya Mecco inayojenga barabara ya Chake-Wete, kufanya uharaka wa kukamilisha Ujenzi wa Barabara hiyo ili kujenga imani ya Wananchi na kuwaondolea usumbufu.

VIONGOZI NA WAKUU WA TAASISI WAMESISITIZWA KUSIMAMIA UWAJIBIKAJI.

Waziri wa Nchi Afisi ya Rais katiba Sheria, Utumishi na Utawala bora Mhe. Haroun Ali Suleiman amesema ni jukumu la wakuu wa Taasisi na vitengo kukaa pamoja kujadili namna ya kuwaelimisha Watendaji wao juu ya utekelezaji wa Sheria ya Utumishi wa Umma.

SERIKALI YA MAPINDUZI ZANZIBAR IMEWATAKA WANANCHI KUENDELEA KUITUNZA MIUNDOMBINU INAYOJENGWA IKIWEMO YA SKULI

Serikali ya Mapinduzi Zanzibar imewataka Wananchi kuendelea kuitunza Miundombinu inayojengwa ikiwemo ya Skuli ili kufikia malengo ya Mapinduzi ya mwaka 1964 ya kutoa elimu bure kwa Wazanzibari katika mazingira yaliyo bora zaidi.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe Hemed Suleiman Abdullah ameyasema hayo alipoweka Jiwe la msingi katika ujenzi wa Skuli ya Sekondari ya Kiwani ikiwa ni muendelezo wa shamra shamra za kutimiza miaka 60 ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Subscribe to MHE HEMED SULEIMAN ABDULLAH
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.