ZANZIBAR YASAINI MRADI WA KUIMARISHA MIUNDOMBINU

NAIBU WAZIRI UJENZI
English

Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imesaini Mkataba wa Miaka Mitano na Czech–Tanzania Development Chamber of Commerce, unaolenga kuimarisha miundombinu na kuchochea uchumi endelevu wa Zanzibar. 

Miongoni mwa Maeneo yatakayotekelezwa ni Sekta ya usafiri wa Anga na Barabara ya Reli na Miradi mingine ya kimkakati ili kuongeza fursa za kiuchumi. 

Kwa upande wa Seikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Saini imetiwa na Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Mhe. Badria Atai Masoud na upande wa Czech–Tanzania Development Chamber of Commerce Saini imetiwa na Pavel Pulec ambae ni Mkurugenzi wa Taasisi hiyo.

Baada ya Utiaji Saini huo, Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi amesema Mkataba huo ni Sehemu ya Mkakati wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar wa kuleta Maendeleo ya haraka kupitia ushirikiano na Wawekezaji wa Kimataifa akibainisha baadhi ya Miradi iliyopangwa kutekelezwa ni kuimarisha Usafiri wa Anga pamoja na uwekezaji katika Miundombinu mingine muhimu.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Czech–Tanzania Development Chamber of Commerce Pavel Pulec amesema Mkataba huo utafungua fursa mpya za Maendeleo Zanzibar.

Serikali inalenga kuchochea Biashara, Utalii na kuongeza Ajira kwa Wananchi hususan Vijana na hatua hii inalenga kuifanya Zanzibar kuwa kitovu cha Usafiri na Biashara Afrika 

 

 

 

Simplenews subscription

The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.