Tanzania Kwa Kushirikiana Na Shirika La Kilimo Na Chakula La Umoja Wa Mataifa (Fao) Imeandaa Mkakati Wa Taifa Wa Zana Za Kilimo Unaolenga Kuimarisha Matumizi Ya Uzalishaji, Usimamizi Na Uratibu Wa Teknolojia Za Kilimo.
Hayo Yamebainishwa Na Waziri Mkuu Wa Tanzania Dk. Mwigulu Lameck Nchemba Katika Mkutano Wa Afrika Kuhusu Matumizi Endelevu Ya Zana Za Kilimo Mkutano Ulienda Sambamba Na Uzinduzi Wa Mkaati Wa Taifa Wa Zana Za Kilimo Wa Awamu Yapili Ambapo Amesema Hali Ya Uwekezaji Katika Zana Za Kilimo Barani Afrika Haiendani Na Mahitaji Halisi Ya Wakulima Wadogo Na Pia Ndio Chanzo Cha Vijana Kukataa Kujikita Katika Sekta Hio.
Kwa Upande Wake Waziri Wa Kilimo Wa Tanzania Mhe. Daniel Chongolo Amesema Mkutano Huu Utatoa Fursa Kwa Tanzania Kupata Uzoefu Wa Maswala Mbalimbali Yanayohusu Namna Bora Ya Kuzalisha Na Matumizi Ya Zana Za Kilimo Kulingana Na Teknolojia Za Kisasa Zinazozingatia Mabadiliko Ya Tabia Nchi.
