WAZIRI MASOUD AWAONYA WATENDAJI WA ZASCO

MHE. MASOUD ALI MOHAMMED
English

Waziri Wa Uchumi Wa Blue Na Uvuvi Zanzibar Mhe. Masoud Ali Mohammed Amewataka Watendaji Wa Kampuni Ya Mwani (Zasco) Kuhakikisha Mipango Waliojiwekea Inakwenda Sambamba Na Malengo Ya Serikali Ya Kuliimarisha Zao Mwani Pamoja Na Kuinua Maslahi Ya Wazalishaji Wa Hilo.

Akizungumza Na Wafanyakazi Wa Zasco Huko Mlandege Mhe. Masoud Amesema Ili Mpango Hupo Uiende Sambamba Na Malengo Ya Serikali Ni Lazima Kuwe Na   Juhudi Za Utekelezaji Kwa Watendaji Wake. 

 

Aidha Waziri Masoud Amesema Katika Kuhakikisha Mikakati Iliyowekwa Na Kampuni Ya Zasco Pamoja Na Malengo Ya Serikali Yanafikiwa Hatosita Kumchukulia Hatua Mtendaji Yoyote Atakae Sababisha Mfarakano Katika Kampuni Hiyo.   

Mkurugenzi Mkuu Wa Kampuni Ya Mwani Zanzibar (Zasco) Dkt. Masoud Rashid Mohammed Amesema Serikali Ya Mapinduzi Ya Zanzibar Imeamua Kuanzisha Kampuni Hiyo Kwa Lengo La Kuboresha Maslahi Ya Wakulima Na Kuongeza Thamani Na Kuimarisha Uwekezaji Wa Zao Hilo. 

Dira Ya Kuwepo Kwa Zasco Ni Kuwa Zao Linalotumainiwa Na Serikali Pamoja Na Wananchi Kwa Ujumla.   

 

Simplenews subscription

The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.