Rais Wa Jamhuri Ya Muungano Watanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan Amesisitiza Vipaumbele Vyenye Umuhimu Kwa Tanzania Na Afrika Kwa Ujumla, Ikiwemo Ustahimilivu Wa Majanga, Uendelevu Wa Madeni, Mpito Wa Haki Wa Nishati Safi, Uongezaji Thamani Wa Madini Muhimu, Na Usalama Wa Chakula.
Rais Samia Ameyasema Hayo Katika Mkutano Wa 39 Wa Wakuu Wa Nchi Na Serikali Wa Umoja Wa Afrika (Au) Unaoendelea Jijini Addis Ababa Ethiopia.
Kauli Ya Rais Samia Ameitoa Aliposhiriki Kikao Cha Umoja Wa Afrika Kuhusu G20, Ambapo Viongozi Walipokea Taarifa Ya Matokeo Ya Mkutano Wa Viongozi Wa G20 Uliofanyika Tarehe 22–23 Novemba 2025.
Kikao Hicho Kilipokea Taarifa Iliyowasilishwa Na Rais Wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa, Ambaye Alifanikiwa Kuandaa Na Kuongoza Mkutano Wa Kwanza Kabisa Wa G20 Kufanyika Katika Ardhi Ya Afrika.
Rais Samia Alimpongeza Rais Ramaphosa Kwa Mafanikio Hayo Aliyoyaeleza Kuwa Ni Ya Kihistoria Kwa Bara La Afrika.
Katika Mkutano Huo Jijini Addis Ababa, Tanzania Imetambuliwa Kuwa Kinara Ambapo Dkt. Samia Suluhu Hassan Ameteuliwa Rasmi Kuwa Bingwa Wa Umoja Wa Afrika (Au) Wa Afya Ya Mama Na Mtoto Kufuatia Mapendekezo Yaliyotolewa Katika Ripoti Ya Mwaka 2025 Ya Kamati Ya Wakuu Wa Nchi Na Serikali Kuhusu Africa Centres For Disease Control And Prevention.
Rais Samia Atahudumu Katika Nafasi Hiyo Kwa Kipindi Cha Mwaka Mmoja Ambapo Atakuwa Na Jukumu La Kuratibu Na Kuhamasisha Juhudi Za Nchi Wanachama Wa Au Katika Kupunguza Vifo Vya Mama Na Mtoto, Kuimarisha Mifumo Ya Afya, Na Kulindahaki Za Afya Ya Uzazi Barani Afrika.
Kando Ya Mkutano Huo, Rais Wa Jamhuri Ya Muungano Watanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan, Amekutana Na Kufanya Mazungumzo Na Naibu Katibu Mkuu Wa Umoja Wa Mataifa Amina Mohamed Jijini Addis Ababa Ethiopia.
Katika Mazungumzo Hayo Rais Samia Ameeleza Dhamira Ya Tanzania Katika Kuendeleza Kutekeleza Mageuzi Ya Kiuchumi Na Kiutawala Pamoja Na Kuimarisha Ushirikiano Wa Nchi Na Umoja Wa Mataifa Katika Kutekeleza Malengo Ya Maendeleo Endelevu Katika Sekta Zianzogusa Maisha Ya Wananchi Ikiwemo Afya, Elimu, Maji Safi Na Kupunguza Umasikini.
Rais Samia Ameonesha Utayari Wa Serikali Katika Wa Serikali Katika Kumpokea Mjumbe Maalum Wa Umoja Mataifa Aliyeomba Kuja Nchini Kwa Ajili Ya Kuwasilisha Ujumbe Maalum Wa Katibu Mkuu Wa Umoja Wa Mataifa, Antonio Guterres.
Kwa Uapnde Wake Naibu Katibu Mkuu Wa Umoja Wa Mataifa Amina Mohamed Amewasilisha Salamu Za Katibu Mkuu Wa Umoja Wa Mataifa Na Kuwa Anathamini Ushirikiano Wa Karibu Uliopo Kati Ya Tanzania Na Umoja Wa Mataifa.
