Habari

ZIARA UKAGUZI WA JENGO LA RAHA LEO WAFIKIA KATIKA HATUA NZURI

    Katibu Mkuu Wizara ya Habari Vijana Utamaduni na Michezo Fatma Hamad Rajab amesema ameridhishwa na Matenegenezo ya jengo la Raha leo ambalo linatarajiwa kuwa Makao Makuu ya Shirika la Utangazaji Zanzibar.

    Ameyasema hayo wakati akifanya Ukagua katika  Jengo la Raha Leo lililotenegenzwa na Serikali ya Jamhuri ya Watu wa China ambapo amesema hatua hiyo itasaidia kuimarisha utendaji kazi wa Shirika la Utangazaji Zanzibar pamoja na kulitaka Shirika hilo kutunza mazingira na Miundombinu ya Jengo hili.

DKT.MWINYI AZIPONGEZA ZAECA NA TAKUKURU KWA KUOKOA FEDHA NA MIRADI YA MAENDELEO NCHINI
ZAWA KUZINDUA MFUMO MPYA WA RASILIMALI MAJI

    Waziri wa Nishati na Madini Mhe.Shaibu Hassan Kaduara amesema Wizara yake itahakikisha inamaliza tatizo la upatikanaji wa huduma ya Maji Zanzibar.

   Akizungumza katika Uzinduzi wa Mifumo wa usimamizi wa Maji  Tazama Maji  katika Ukumbi wa Zawa Madema  amesema hatua hiyo itaweza kuijulisha Mamlaka sehemu yenye kima kidogo ama kikubwa cha Maji na kutafutiwa ufumbuzi wake.

ZAIDI YA AJIRA ELFU SABA KUPATIKANA KUTOKANA NA UWEKEZAJI WA VISIWA

      Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dkt.Hussein Ali Mwinyi amesema uamuzi wa kukodisha visiwa kwa uwekezaji wa muda mrefu ulikuwa uamuzi wa kimkakati ambao na kusababisha kusajiliwa kwa miradi 16 yenye thamani ya dola za kimarekani milioni 384 za uwekezaji mtaji na kutoa ajira zaidi ya 7,000 kwa wenyeji.

      Rais Dkt.Mwinyi aliyasema hayo tarehe 11 Juni 2024, alipofungua Jukwaa la Uwekezaji na Uhifadhi wa Bahari Zanzibar katika ukumbi wa Hoteli ya Golden Tulip Airport, Mkoa wa Mjini Magharibi.

TANZANIA KUIMARISHA SEKTA YA UZALISHAJI SUKARI

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt.Hussein Ali Mwinyi amesema, Tanzania sekta ya Sukari ni kipaumbele katika ukuzaji wa maendeleo ya  Viwanda Nchini . 

Dkt.Mwinyi ameyasema hayo alipofungua Mkutano wa Wazalishaji Sukari wa Nchi za SADC katika ukumbi wa Hoteli ya Golden Tulip  iliopo Uwanja wa ndege Zanzibar.

DKT. MPANGO AMETAKA UHARAKISHWAJI WA VITAMBULISHO VYA TAIFA

Makamu wa Rais amesema hayo wakati akizungumza na Wananchi wa eneo la Mnanila akiwa katika ziara Mkoa wa Kigoma. Amesema kukosekana kwa Vitambulisho hivyo kunawanyima fursa mbalimbali Wananchi hao ikiwemo kukosa Ajira katika Miradi inayotekelezwa Mkoani humo.

Katika hatua nyingine Makamu wa Rais amezungumza na Wananchi wa Kijiji cha kalinzi kilichopo Wilaya ya Kigoma ambapo amewasihi kulinda na kutunza Amani iliyopo Nchini na katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa ili kuhakikisha Wanachagua Viongozi bora watakaowatumikia vema.

TAASISI ZA URITHI NA MAMBO YA KALE ZIMETAKIWA KUSIMAMIA MAPATO

Waziri wa Utalii na mambo ya Kale Zanzibar Mhe. Mudrik Ramadhan Soraga ameziagiza Mamlaka husika zinazosimamia Urithi na mambo ya kale Zanzibar kuhakikisha wanasimamia mapato ya Serikali kupitia Sekta hizo.

Waziri Soraga akizungumza kwa wakati tofauti katika ziara ya kukaguwa Sekta hizo amesema maeneo hayo yana umuhimu mkubwa katika kuchangia pato la Taifa hivyo amewataka Wakurugenzi Dhamana kuhakikisha wanakaa na Wawekezaji ili kutimiza wajibu wao katika kuchangia pato la Taifa kama walivyo kubaliana katika Mikataba yao.

MKOA WA GEITA UMEVUKA ONGEZEKO LA IDADI YA WATU TAIFA KWA ASILIMIA 5%,

Kufuatia ongezeko la idadi kubwa ya Watu Mkoani Geita ambalo linavuka ongezeko la idadi ya Taifa kwa Asilimia 5%, kilele cha Maadhimisho ya Siku ya idadi ya Watu Duniani Kitaifa yatafanyika Mkoani humo kesho.

Mkoa wa Geita una Watu Mil. 2 na Laki 9 huku Kitaifa ikiwa ni Mil. 61 wakati kasi ya ukuaji wa idadi ya Watu mkoa wa Geita ni 5.4% wakati Kitaifa kasi ya ukuaji wa idadi ya Watu 3.2% hivyo Mkoa wa Geita idadi ya Watu inakua kuliko wastani wa Kitaifa, Afisa mipango Tume ya Mipango Zanzibar, Umrat Suleiman amezungumzia kuelekea Siku hiyo.

WANANCHI WAMESISITIZWA KUUNGA MKONO JUHUDI ZA SERIKALI

Mhadhiri wa Kimataifa wa dini ya Kiislamu Dk. Sheikh Seif Hassan Sulleiman amemtaja Rais Samia Suluhu Hassan kama mmoja wa viongozi wa mfano na kuigwa Duniani katika Diplomasia ya kisiasa.

Ni katika Viwanja vya furahisha Jijini Mwanza, ambako Waumini wa Dini ya Kiislamu Wanashiriki kongamano la Siku Kumi la Maadili na unasihi lililoandaliwa na Baraza kuu la Waislamu Tanzania Bakwata Mkoani hapa.

Mgeni Rasmi katika shughuli hiyo ni Mhadhiri wa kimataifa wa Dini ya kiislamu Sheikh Dkt. Seif Hassan Sulle kutoka Dar es salaam.

Subscribe to Habari
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.