TAASISI ZA URITHI NA MAMBO YA KALE ZIMETAKIWA KUSIMAMIA MAPATO

MHE. MUDRIK RAMADHAN SORAGA

Waziri wa Utalii na mambo ya Kale Zanzibar Mhe. Mudrik Ramadhan Soraga ameziagiza Mamlaka husika zinazosimamia Urithi na mambo ya kale Zanzibar kuhakikisha wanasimamia mapato ya Serikali kupitia Sekta hizo.

Waziri Soraga akizungumza kwa wakati tofauti katika ziara ya kukaguwa Sekta hizo amesema maeneo hayo yana umuhimu mkubwa katika kuchangia pato la Taifa hivyo amewataka Wakurugenzi Dhamana kuhakikisha wanakaa na Wawekezaji ili kutimiza wajibu wao katika kuchangia pato la Taifa kama walivyo kubaliana katika Mikataba yao.

Aidha Waziri Soraga ametoa agizo kwa Mamlaka hizo kuongeza nguvu katika Ulinzi hasa eneo la Fungu la nakupenda ili kuzuia athari zinazotokana na uchafuzi wa Mazingira unaosababishwa na Watumizi wa eneo hilo.

Wamiliki na Watumiaji wa maeneo yaliyokaguliwa wamesema watayafanyia kazi maagizo ya Serikali huku wakiomba usimamizi katika maeneo yao dhidi watu wanaofanya uharibifu.

Katika ziara hiyo Waziri wa Utalii ametembelea Kisiwa cha Prison, fungu la nakupenda na Bustani ya Mbweni.

stories
standard
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.