Kufuatia ongezeko la idadi kubwa ya Watu Mkoani Geita ambalo linavuka ongezeko la idadi ya Taifa kwa Asilimia 5%, kilele cha Maadhimisho ya Siku ya idadi ya Watu Duniani Kitaifa yatafanyika Mkoani humo kesho.
Mkoa wa Geita una Watu Mil. 2 na Laki 9 huku Kitaifa ikiwa ni Mil. 61 wakati kasi ya ukuaji wa idadi ya Watu mkoa wa Geita ni 5.4% wakati Kitaifa kasi ya ukuaji wa idadi ya Watu 3.2% hivyo Mkoa wa Geita idadi ya Watu inakua kuliko wastani wa Kitaifa, Afisa mipango Tume ya Mipango Zanzibar, Umrat Suleiman amezungumzia kuelekea Siku hiyo.
Ramadhani Hangwa Mchambuzi wa masuala ya idadi ya Watu na maendeleo kutoka Shirika la umoja wa Mataifa la idadi ya Watu (unfpa) amezungumzia umuhimu wa maadhimisho ya Siku hiyo.
Mchambuzi wa masuala ya idadi ya Watu na maendeleo kutoka Shirika la umoja wa Mataifa la idadi ya Watu (unfpa),
Shirika la lisilo la Kiserikali la Marie Stopes Tanzania kupitia kwa Mkuu wake wa Uchechemuzi Oscar Kimaro, amezungumzia juu ya umuhimu wa Takwimu sahihi katika kukuza Maendeleo.