Makamu wa Rais amesema hayo wakati akizungumza na Wananchi wa eneo la Mnanila akiwa katika ziara Mkoa wa Kigoma. Amesema kukosekana kwa Vitambulisho hivyo kunawanyima fursa mbalimbali Wananchi hao ikiwemo kukosa Ajira katika Miradi inayotekelezwa Mkoani humo.
Katika hatua nyingine Makamu wa Rais amezungumza na Wananchi wa Kijiji cha kalinzi kilichopo Wilaya ya Kigoma ambapo amewasihi kulinda na kutunza Amani iliyopo Nchini na katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa ili kuhakikisha Wanachagua Viongozi bora watakaowatumikia vema.
Vilevile Makamu wa Rais amezungumza na Wananchi wa Wilaya ya Buhigwe ambapo amewahakikishia kwamba Serikali inaendelea kuboresha Miundombinu ya Mkoa wa Kigoma ili kuwawezesha Wananchi kufanya shughuli za Kiuchumi kirahisi ikiwemo Biashara.
Waziri wa ujenzi innocent Bashungwa amewaahidi Wananchi wa Kigoma kuwakabidhi Barabara ya Kasulu – Buhigwe hadi Manyovu na Barabara ya Kasulu Kibondo ifikapo Mwezi machi 2025 ili kurahisisha shughuli za Kibiashara na uwekezaji Mkoa wa Kigoma.