Habari

MWALIMU AHUKUMIWA MIAKA 30 JELA KWA KUINGILIWA KINYUME NA MAUMBILE NA MWANAFUNZI

     Mwalimu wa kiume afahamikae kwa jina la Ramadhan Said Nanyalika (32) Mkazi wa Mtaa wa Matogoro, Tandahimba Mjini Mkoani Mtwara amehukumiwa kwenda jela miaka 30 baada ya kuruhusu kuingiliwa kinyume na maumbile, Mwalimu huyo amekuwa akifundisha Shule ya Sekondari Naputa kwa kipindi kirefu sasa.

    Kamanda wa Polisi wa Polisi Mkoa wa Mtwara SACP, Issa Suleiman ametoa taarifa hiyo Julai 09, 2024

DKT.MPANGO ATAKA MSUKUMO UTOLEWA KWA VIJIJI NA VITONGOJI VISIVYO NA UMEME

     Makamu wa Rais, Mhe. Dkt Philip Isdor Mpango ambaye yupo katika ziara ya kukagua miradi ya maendeleo  mkoani Kigoma, ameiagiza Wizara ya Nishati kuhakikisha kuwa inatoa msukumo wa upatikanaji  umeme  kwa vijiji na vitongoji ambavyo bado havijafikiwa na huduma hiyo.

   Dkt Mpango ameyasema hayo wakati akikagua miradi mbalimbali inayotekelezwa na Serikali mkoani Kigoma ikiwa ni siku ya pili ya ziara yake mkoani humo.

WAZIRI JAFO SITAKUBALI JUHUDI ZA RAIS SAMIA KWENYE SEKTA YA VIWANDA ZIKWAMISHWE

Waziri wa Viwanda na Biashara, Dkt. Selemani Jafo hakurizishwa na kiwango cha Watanzania kutumia Mbolea ya kiwanda ya cha Intracom kilichopo nala Jijini Dodoma.

 Akizungumza na Waandishi wa Habari mara baada ya kufanya  Ziara kwenye kiwanda hicho, Waziri Jafo amesema kuwa kina uwezo wa  kuzalisha Tani Milioni moja kwa Mwaka na mahitaji ya mbolea kwa mujibu wa Wizara ya Kilimo ni Tani 700,000 na kwamba Kiwango kilichozalishwa kwasasa Takwimu zinaonesha kiwango kidogo kimeuzwa Nchini.

WIZARA YA UJENZI KAMILISHA UJENZI WA BARABARA KWA KIWANGO CHA LAMI MALAGARASI – UVINZA

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango ameiagiza Wizara ya Ujenzi kuhakikisha inakamilisha Ujenzi wa Barabara kwa kiwango cha Lami Malagarasi – Uvinza   ifikapo Mwezi Machi 2025 kama ilivyopangwa.

Makamu wa Rais ametoa maelekezo hayo mara baada ya kukagua maendeleo ya Ujenzi wa Barabara hiyo akiwa Ziara Mkoani Kigoma. 

Amewasihi Viongozi na Watendaji kuhakikisha Wanasimamia  Barabara hiyo ili iweze kukamilika kwa wakati na kuwawezesha Wananchi kushiriki vema shughuli za Kiuchumi na Ujenzi wa Taifa.

WASANIFU ,WAHANDISI NA WAKADIRIAJI MAJENGO WATAKIWA KUFUATA SHERIA NA KANUNI KUWEZA KUJISAJILI

Bodi ya usajili, Wasinifu, Wahandisi na Wakadiriaji majengo Zanzibar  imewataka Wataalamu kufuata sheria na kanuni zinazowaongoza ili kuweza kujisajili kwa Lengo la kufanyakazi zao kwa Ubunifu na ufanisi kwa mslahi ya Wananchi na Taifa.

ZANZIBAR YATEKETEZA DAWA ZA KULEVYA

Mamlaka ya kudhibiti na kupambana na Dawa za kulevya imeteketeza Dawa za Kulevya aina mbalimbali ikiwemo Heroine, Bangi, Mirungi na Valiamu.

Akizungumza katika zoezi la uteketezaji wa Dawa hizo huko Mahonda kamishna wa Mamlaka ya kudhibiti na kupambana na Dawa za Kulevya Kanali Burhani Zuberi Nassor amesema Dawa hizo ambazo  kesi zake zimeshaisha tokea Mwaka 2018 hadi 2024 na wanaokamatwa na Dawa hizo  mali zao zinataifishwa.

WATANZANIA WATAKIWA KUCHANGAMKIA FURSA ZA MATAIFA YA KIGENI KATIKA MAONESHO YA SABASABA

Washiriki wa Maonesho ya 48 ya Biashara ya Kimataifa Dar Es Salaam (Sabasaba) wametakiwa kushirikia katika Siku maalum zizoandaliwa katika maonesho hayo ili Kuweza kujifunza fursa mbalimbali za uwekezaji kutoka Mataifa ya nje ya Nchi.

Kauli hiyo imetolewa na Mkurugenzi mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (Tantrade) Bi Latifa Mohamed Khamis katika wa Siku maalum kwa ajili ya Taifa  la Iran katika maonesho hayo.

Amesema wameandali Siku hiyo ili kuweza kuangalia fursa zilipo katika Mataifa mengine pamoja na kuzitangaza fursa  za uwekezaji zilizopo Nchi.

KIWANDA CHA SUKARI MKULAZI MOROGORO KUANZA KUZALISHA SUKARI

    Baada ya Majaribio ya Kuzalisha Sukari Mwaka Jana katika Kiwanda cha Sukari Mkulazi kilichopo Wilaya ya Kilosa Mkoani Morogoro, Kiwanda hicho kwa sasa kimeanza rasmi uzalishaji wa Sukari  Julai Mosi Mwaka huu ambapo mpaka sasa Tani zaidi ya Miatatu zimezalishwa na kuanza kuingia Sokoni.

   Hayo yamebainishwa na Meneja wa Kiwanda cha Sukari Mkulazi Mhandisi Aron Mwaigaga mara baada ya Kamati ya Usalama Wilaya Kilosa ikiongozwa na Mkuu wa Wilaya hii Bwana Shaka Hamdu Shaka kufika na kujionea Uzalishaji huo ulivyoanza.

WAISLAMU ZANZIBAR WAADHIMISHA MWAKA MPYA WA KIISILAMU

    Waislamu wa Maeneo Mbalimbali Zanzibar wamejitokeza katika Matembezi ya maadhimisho ya Mwaka Mpya wa  Kiislamu huku Viwanja vya Mnazi Mmoja.

    Akipokea Matembezi ya Mwaka Mpya wa Kiislam  Spika wa Baraza la Wawakilishi Mhe.Zuberi Ali Maulid amesema Maadhimisho hayo yanakumbusha Safari ya Mtume wakati alipohama Makka kuelekea Madina hivyo Waumini wa Kiislamu na Watu wengine wana mengi ya kujifunza  katika kutekeleza maamrisho ya Mwenyezi Mungu.

HALMASHAURI KUU YA CCM KASKAZINI UNGUJA IMERIDHISHWA NA RIPOTI TEKELEZAJI YA ILANI YA CHAMA

    Halmashauri Kuu ya CCM  Mkoa wa Kaskazini Unguja imesema imeridhishwa na Ripoti tekelezaji ya ilani ya Chama cha Mapinduzi  iliyofanywa na Serikali ya Mkoa huo.

    Ameyasema hayo Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Kaskazini Unguja  Iddi Ali Ame  katika Kikao cha kuskiliza  Taarifa ya hali ya kisiasa na utekelezaji wa ilani ya Chama kilichofanyika katika Ofisi za Chama hicho  Mahonda.

Subscribe to Habari
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.