Halmashauri Kuu ya CCM Mkoa wa Kaskazini Unguja imesema imeridhishwa na Ripoti tekelezaji ya ilani ya Chama cha Mapinduzi iliyofanywa na Serikali ya Mkoa huo.
Ameyasema hayo Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Kaskazini Unguja Iddi Ali Ame katika Kikao cha kuskiliza Taarifa ya hali ya kisiasa na utekelezaji wa ilani ya Chama kilichofanyika katika Ofisi za Chama hicho Mahonda.
Amesema Kikao hicho kinaumuhimu kwa Chama na Wananchi kwa Ujumla kwani kinahakikisha walichoahidiwa Wananchi kupitia Kampeni za Uchaguzi kimetekelezeka kwa wakati.
Akiwasilisha Taarifa ya utekelezaji wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi Mkuu wa Mkoa Kaskazini Unguja Mhe.Rashid Hadidi Rashid amesema Serikali imekamilisha utekelezaji katika Sekta mbali mbali katika Mkoa huo ikiwemo Afya, Miundombinu, Kilimo na Elimu ambavyo hadi sasa vimeweza kuufanya Mkoa huo kuwa na kasi kubwa ya Maendeleo
Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo, Umwagiliaji ,Mali Asili na Mifugo Zanzibar Ndg.Ali Khamis Juma amesema Wizara ya Kilimo itahakikisha kuanzia Mwezi wa Julai hadi Disemba wanafanya mageuzi ya Kilimo ili kuonyesha fursa za Kilimo Wananchi .
Nao Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Mkoa wa Kaskazini Unguja wamekishuru Chama cha Mapinduzi kwa kubuni Vikao vya kusikiliza utekelezaji wa Ilani ya Chama kwani vitaisadia kuiwajibisha Serikali kutatua matatizo mbali mbali za Wananchi katika Jamii.
Kikao hicho cha Halmashauri Kuu ya CCM Mkoa wa Kaskazini Unguja hufanyika kila Baada ya Miezi Sita ambapo huangalia utekelezaji wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi CCM.