Habari

WAZIRI SHARIF AZINDUWA MAANDALIZI YA IJITMAI YA KIMATAIFA KIDOTI

   Waziri wa Nchi Ofisi ya Raisi  Kazi Uchumi na Uwekezaji Mhe.Sharif Ali Sharif amewataka  Waumini wa Dini ya Kiislam kutoa mali zao na nafsi zao kwaajili ya kupeleka mbele harakati za Kiislam ili kuitengeneza Jamii yenye maadili mema .

    Akizungumza katika Uzinduzi wa harakati za Ijitamia ya Kimataifa ambayo Mwaka huu inatarajiwa kufanyia Kidoti Mkoa wa Kaskazini Unguja Mhe.Sharif amesema  Taasisi za Kidini zina mchango mkubwa katika kuhuisha  maadili mema katika Jamii . 

TAWA YATUMIA MAONESHO YA SABASABA KUNADI FURSA LUKUKI ZA UWEKEZAJI

     Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA) inatumia maonesho ya 48 ya kimataifa ya kibiashara yanayoendelea Jijini Dar es Salaam kuhamasisha Umma wa watanzania wawekezaji na wageni  kutoka mataifa mbalimbali kuwekeza katika maeneo  inayoyasimamia huku ikijinasibu kuwa na fursa lukuki za uwekezaji

BURUDANI ,MAPISHI NA MIJADALA VYANOGESHA USIKU WA KISWAHILI COMORO

     Watanzania waishio nchini Comoro na wananchi wa Kisiwa cha Ngazija na wanadiplomasia wameshiriki katika maadhimisho ya Siku ya Kiswahili Duniani kwa burudani mbali mbali pamoja na mijadala.

    Takribani washiriki 500 wamejitokeza katika Ukumbi wa Bunge la nchi hiyo ambapo nyimbo za kitanzania,mashairi na maigizo vilipamba shughuli hiyo.

PBZ YAKABIDHI GAWIO LA BIL.7 KWA SERIKALI YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR

     Benki ya Watu wa Zanzibar (PBZ) imekabidhi gawio la Sh 7 Bilioni kwa mwanahisa wake wa pekee Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) kufuatia faida iliyopata katika kipindi cha mwaka 2023. Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inamiliki asilimia 100 ya hisa za benki hiyo.

RAIS SAMIA AMUAGA RAIS WA MSUMBIJI.

Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mh Samia Suluhu Hassan  akimuaga Rais wa Msumbiji Filipe Jacinto Nyusi katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abedi amani.

Katika Uwanja wa Ndege Viongozi mbali mbali wa Chama na Serikali wamehudhulia kumuaga Rais Nyusi.

Vikundi mbali mbali vya Utamaduni vimetumbuiza katika kumuaga Rais huyo.

RAIS WA ZANZIBAR AMESEMA UDUGU ULIOPO KATI YA MSUMBIJI NA TANZANIA NI WA KULETA MAENDELEO.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi amesema udugu uliopo kati ya Msumbiji na Tanzania ni wa kuleta Maendeleo Baina ya Nchi mbili hizo hivyo ni vyema kuthaminiwa kwa Vizazi vijavyo.

Akizungumza mara baada ya kukutana na Rais wa Jamhuri ya Msumbiji Mhe. Filipe Jacinto Nyusi aliyefika kumuaga Dk Mwinyi baada ya kumaliza ziara Nchini Tanzania. 

Dk. Mwinyi amesema amefurahishwa na ujio wa Rais huyo pamoja na kuitembelea Zanzibar. 

DKT. MWINYI KUKUTANA NA MAKAMU WA RAIS WA BENKI YA UWEKEZAJI YA UMOJA WA ULAYA.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt.Hussein Ali Mwinyi amekutana na Makamu wa Rais wa Benki ya uwekezaji ya umoja wa Ulaya Thomas Ostros na ujumbe wake, kwa mazungumzo huko Ikulu Zanzibar

Katika mazungumzo hao Rais Mwinyi amezungumzia masuala mbalimbali yakiwemo ya Uchumi wa Buluu, Sekta ya Uvuvi na ya Wajasiriamali  wakiwemo akina Mama wanaojishughulisha na Ulimaji wa Mwani,Uimarishaji wa Bandari ya Mangapwani,pamoja na masuala ya Nishati ya Umeme.

KUMALIZA MARADHI YASIOAMBUKIZA YANAHITAJI NGUVU NA WADAU

Waziri  wa Afya Zanzibar Nassro Ahmed Mazrui amesema mapambano ya kumaliza Maradhi yasioambukiza Zanzibar yanahitaji nguvu ya pamoja na Wadau ili kuwa na Taifa Salama lisilo na Maradhi. Mhe, Mazrui amebainisha hayo katika mkutano wa Wadau wa kujadili mbinu za kumaliza mara Maradhi yasiyoambukiza

Amesema mabadiliko ya Mtindo wa Maisha ndio chanzo cha Magonjwa yasiyoambukiza ikiwemo kutokufanya mazoezi ya Kutosha na tabia bwete ambyo husababisha kuongezeka kwa uzito wa Mwili

WAKANDARASI WANAOJENGA MIRADI YA MAENDELEO KUHESHIMU MIKATABA YA MAKUBALIANO.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe Hemed Abdallah amewataka Wakandarasi wanaojenga Miradi ya maendeleo kuheshimu Mikataba ya makubaliano kati ya Serikali na Kampuni husika.       

Akizungumza katika Ziara ya kutembelea na kukagua Maendeleo ya Ujenzi wa Jengo la Ofisi Kuu ya Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) Maisara Mhe. Hemed amesema baadhi ya Wakandarasi huchelewesha kumaliza Miradi kwa wakati na kuomba kuongezewa muda jambo ambalo linakwamisha adhma ya Serikali ya kutatua kero za Wananchi kwa wakati. 

VIONGOZI WA DINI WAMETAKIWA KUHUBIRI AMANI.

Naibu Kadhi Mkuu wa Zanzibar Shekhe Othman Ame Choum amewataka Viongozi wa Dini kuendelea kuhubiri Amani kwa lengo la kukuza uchumi na kuleta maedneleo Nchini.

Naibu Kadhi huyo ameseyasema hayo huko Gombani katika Kongamano la

Kuukaribisha Mwaka Mpya wa Kiislamu 1446 Hijria ,lililowakutanisha Viongozi na Waumini wa Dini ya Kiislamiu .

Amesema suala la uvunjifu wa Amani silakupewa nafasi kutokana na kuwepo kwa Athari kubwa katika Jamii kiuchumi na Kimaendeleo hivyo ni jukumu la Waislam  Kuendelea kutunza amani kwa faida yao na Taifa.

Subscribe to Habari
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.