RAIS WA ZANZIBAR AMESEMA UDUGU ULIOPO KATI YA MSUMBIJI NA TANZANIA NI WA KULETA MAENDELEO.

RAIS WA SERIKALI YA MAPINDUZI ZANZIBAR

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi amesema udugu uliopo kati ya Msumbiji na Tanzania ni wa kuleta Maendeleo Baina ya Nchi mbili hizo hivyo ni vyema kuthaminiwa kwa Vizazi vijavyo.

Akizungumza mara baada ya kukutana na Rais wa Jamhuri ya Msumbiji Mhe. Filipe Jacinto Nyusi aliyefika kumuaga Dk Mwinyi baada ya kumaliza ziara Nchini Tanzania. 

Dk. Mwinyi amesema amefurahishwa na ujio wa Rais huyo pamoja na kuitembelea Zanzibar. 

Rais wa Msumbiji Filipe Jacinto Nyusi akiwa na Ujumbe wake ametoa salamu za pole kufuatia Kifo cha Rais Mstaafu wa Zanzibar wa awamu ya Tatu na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Hayati Mzee Ali Hassan Mwinyi na kumualika Dk. Mwinyi kutembelea Msumbiji kabla ya kumaliza muda wake Madarakani.

Msumbiji inatarajiwa kufanya Uchaguzi Mkuu wa Rais Mwezi Oktoba Mwaka huu.

stories
standard
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.