KUMALIZA MARADHI YASIOAMBUKIZA YANAHITAJI NGUVU NA WADAU

WAZIRI WA AFYA ZANZIBAR

Waziri  wa Afya Zanzibar Nassro Ahmed Mazrui amesema mapambano ya kumaliza Maradhi yasioambukiza Zanzibar yanahitaji nguvu ya pamoja na Wadau ili kuwa na Taifa Salama lisilo na Maradhi. Mhe, Mazrui amebainisha hayo katika mkutano wa Wadau wa kujadili mbinu za kumaliza mara Maradhi yasiyoambukiza

Amesema mabadiliko ya Mtindo wa Maisha ndio chanzo cha Magonjwa yasiyoambukiza ikiwemo kutokufanya mazoezi ya Kutosha na tabia bwete ambyo husababisha kuongezeka kwa uzito wa Mwili

Meneja Mradi wa Pharm Access Dkt faiza Abasi amesema Maradhi yasiyoambukiza yameathiri Watu wengi  hali inayosababisha  kupoteza nguvu kazi ya Jamii.

Akiwasilisha mada juu ya Maradhi  hayo Mwenyekiti Ncd Alliance Tanzania Prof Andrew Swai amesema ni wajibu wa kila mtu kuacha tabia ya kula Vyakula vya Nafaka vilivyokobolewa Pamoja na Ukamuaji wa Matunda

Ugonjwa wa Moyo unaongoza  kwa Vifo vingi zaidi Duniani  Ukifatiwa na Saratani, Kisukari nafasi ya Tatu.

stories
standard
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.