Waziri wa Afya Zanzibar Nassro Ahmed Mazrui amesema mapambano ya kumaliza Maradhi yasioambukiza Zanzibar yanahitaji nguvu ya pamoja na Wadau ili kuwa na Taifa Salama lisilo na Maradhi. Mhe, Mazrui amebainisha hayo katika mkutano wa Wadau wa kujadili mbinu za kumaliza mara Maradhi yasiyoambukiza
Amesema mabadiliko ya Mtindo wa Maisha ndio chanzo cha Magonjwa yasiyoambukiza ikiwemo kutokufanya mazoezi ya Kutosha na tabia bwete ambyo husababisha kuongezeka kwa uzito wa Mwili
Meneja Mradi wa Pharm Access Dkt faiza Abasi amesema Maradhi yasiyoambukiza yameathiri Watu wengi hali inayosababisha kupoteza nguvu kazi ya Jamii.
Akiwasilisha mada juu ya Maradhi hayo Mwenyekiti Ncd Alliance Tanzania Prof Andrew Swai amesema ni wajibu wa kila mtu kuacha tabia ya kula Vyakula vya Nafaka vilivyokobolewa Pamoja na Ukamuaji wa Matunda
Ugonjwa wa Moyo unaongoza kwa Vifo vingi zaidi Duniani Ukifatiwa na Saratani, Kisukari nafasi ya Tatu.