DKT. MWINYI KUKUTANA NA MAKAMU WA RAIS WA BENKI YA UWEKEZAJI YA UMOJA WA ULAYA.

RAIS WA SERIKALI YA MAPINDUZI ZANZIBAR

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt.Hussein Ali Mwinyi amekutana na Makamu wa Rais wa Benki ya uwekezaji ya umoja wa Ulaya Thomas Ostros na ujumbe wake, kwa mazungumzo huko Ikulu Zanzibar

Katika mazungumzo hao Rais Mwinyi amezungumzia masuala mbalimbali yakiwemo ya Uchumi wa Buluu, Sekta ya Uvuvi na ya Wajasiriamali  wakiwemo akina Mama wanaojishughulisha na Ulimaji wa Mwani,Uimarishaji wa Bandari ya Mangapwani,pamoja na masuala ya Nishati ya Umeme.

Makamu wa Rais wa Benki ya uwekezaji ya umoja wa Ulaya ameelezea kuridhishwa na mwenendo wa Wajasiriamali wadogo na wakati katika Sekta ya Uchumi wa Buluu walionufaika kupitia mfuko uliozishirikisha Benki za Tanzania wanavyoendelea na shughuli zao.

stories
standard
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.