JAPAN NA ZANZIBAR ZAAHIDI KUSHIRIKIANA

MH HEMED SULEIMAN ABDULLA
English

Makamu Wa Pili Wa Rais Wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla Amesema Serikali Ya Mapinduzi Ya Zanzibar Itaendeleza Uhusiano Ulipo Kati Ya Serikali Ya Japan Na Zanzibar Uliodumu Kwa Muda Mrefu.

Mhe. Hemed Ameyasema Hayo Alipofanya Mazungumzo Na Balozi Wa Japan Nchini Tanzania Yoichi Mikami Afisini Kwake Vuga Zanzibar.

Amesema Uhusiano Uliopo Kati Ya Tanzania Na Japan Utaendelea Kukuza Ushirikiano Katika Pande Zote Mbili Katika Kuimarisha Sekta Za Kilimo, Biashara, Maji Safi Na Salama, Maendeleo Ya Viwanda, Utalii Na Miundombinu Mbali Mbali.

Mhe. Hemed Amemuhakikishia Balozi Mikami Kuwa Serikali Ya Mapinduzi Ya Zanzibar Itaendelea Kushirikiana Na Serikali Ya Japan Katika Sekta Mbali Mbali Hasa Katika Sekta Za Kimkakati Zinazolenga Kuimarisha Diplomasia Ya Kiuchumi.

Kwa Upande Wake Balozi Wa Japan Nchini Tanzania Yoichi Mikami Ameipongeza Serikali Ya Mapinduzi Ya Zanzibar Kwa Kupiga Hatua Katika Nyanja Za Kiuchumi Na Kijamii Na Kwamba Ameahidi Kuendeleza Ushirikiano Ulipo Kati Ya Tanzania Na Japan.

 

Simplenews subscription

The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.