Habari

RAIS FILIPE NYUSI AFUNGUA MAONESHO YA 48 YA SABASABA

Rais wa Jamhuri ya Msumbiji Filipe Jacinto Nyusi amefungua maonesho ya 48 ya Biashara ya kimataifa dar es salaam (sabasaba) 2024 huku akiwataka Washiriki wa maonesho hayo kuto jifungia ndani na badala yake kutafuta fursa za Masoko nje ya Nchi.

Akihutubia katika hafla ya ufunguzi wa maonesho hayo akiwa Mgeni Rasmi Rais Nyusi ambaye yupo Nchini kwa ziara ya Siku Nne amewataka Wafanyabiashara wa Msumbiji na Tanzania kuendelea kushiriki ili kuweza kukuza Biashara zao.

Awali Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia

MASHEHA NA MADIWANI KUYASIMAMIA VYEMA MAENEO YAO

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa, Serikali za Mitaa na idara maalum za SMZ  ,Mhe Masoud Ali Mohamed, amewasisitiza Masheha na Madiwani kuyasimamia vyema maeneo yao, ili kuimarisha ulinzi na usalama katika shehia zao.

Akizungumza na masheha, madiwani na Watendaji wa Wilaya ya Kusini huko Makunduchi, amesema kuwepo kwa Mikakati imara watakayoyaanzisha kutasaidia pia kuvidhibiti Vikundi vya uhalifu na Wananchi pamoja na Wageni wataendelea kuishi katika hali ya usalama.

MASHEHA WAMETAKIWA KUJUA HAKI NA WAJIBU WAO KWA WANANCHI

Tume ya Haki  za Binadamu na Utawala bora Tanzania imeendelea kutoa Mafunzo kwa Masheha wa Wilaya ya Mjini  yatakayowasadia katika kuwajengea uwelewa   wa kusimamia majukumu ya kazi zao za kuwahudumia Wananchi.

Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Idrissa Kitwana Mustafa amewataka Masheha hao kusimamia vyema na watekelze Majukumu yao  kwa kujua nafasi ya haki za Binadamu na wajibu wao katika mazingira yao ya kazi na Jamii kwa ujumla na kufuata misingi ya haki, Kanuni na Utawala bora katika Jamii.

SERIKALI YAFANYA UWEKEZAJI KWENYE SEKTA YA AFYA

Mkurugenzi Mkuu wa Bohari ya Dawa Tanzania MSD Mavere Tukai amesema uwekezaji mkubwa unaofanywa na Serikali katika sekta ya Afya Nchini umechangia kuimarika kwa upatikanaji wa huduma na Bidhaa za afya.

Mkurugenzi Tukai amebainisha hayo wakati akizungumza na Wahariri na Waandishi wa Habari baada ya kukamilika kwa Ziara ya Wahariri ya kutembelea Ghala la MSD Kanda ya Dodoma.

SMT NA SMZ KUIMARISHA ELIMU BORA

Serikali ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar zimeamua kuimarisha Mazingira bora ya  Elimu ya juu kwa Wananchi wake.

Akizindua mradi wa Elimu ya juu kwa mageuzi ya kiuchumi Nchini Tanzania katika Taasisi ya Sayansi ya bahari huko Chukwani Naibu Mratibu wa Mradi huo Dkt liberato Haule amesema lengo la Mradi huo ni juhudi za Serikali za kuhakikisha wanaongeza mchango wa Elimu ya juu kwa maendeleo ya Uchumi wa Taifa.

TUME YA UTANGAZAJI KUPATIWA MAFUNZO YA KUZUIA PICHA ZILIZO KINYUME NA MAADILI

Tume ya Utangazaji Zanzibar imesema imeandaa Mafunzo ya kuwapatia Watumishi wa Tume hiyo kutoka Mamlaka ya mawasiliano TanzaniaTCRA ili kuwapatia uwezo wa kuzuia Picha zilizo kinyume na maadili kusambazwa katika Mitandao

Akizumgumza na ZBC Katibu Mtendaji wa Tume hiyo Bw Suleiman Abdulla Salim   amesema hatua hiyo itasaidia kupunguza na kuondosha Mmomonyoko wa Maadili Nchini.

WAZIRI MKUU ATAKA USHIRIKIANO KATI YA SERIKALI NA TAASISI ZA DINI KUZIDI KUIMARISHWA

     Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan anasisitiza ufanyaji kazi kwa ushirikiano kati ya Serikali na Taasisi za Dini nchini ili kuendelea kujenga amani, umoja na mshikamano.

    Amesema kuwa Serikali inatambua mchango mkubwa unaotolewa na Taasisi hizo ambao huleta matokeo chanya kwa ustawi wa Taifa.

REA KUHAKIKISHA VIJIJI VYOTE TANZANIA KUFIKIWA NA NISHATI YA UMEME

     Naibu Waziri wa Nishati, Mhe. Judith Kapinga ameeleza kuwa, Serikali kupitia Wakala wa Nishati Vijijini ( REA) inatekeleza Mradi wa Kusambaza Umeme Vijijini kwa Awamu tofauti ambapo vijiji vyote ambavyo havina umeme Tanzania Bara vitafikiwa na huduma ya umeme.

    Ameeleza hayo leo Tarehe 2, Julai 2024 alipokuwa katika muendelezo wa ziara yake ya kukagua miradi ya umeme katika Vijiji vya Buganzo, Gura na Mwakata vilivyopo katika Jimbo la Msalala Wilaya ya Kahama.

ZANROAD NA TANROAD YAINGIA MAKUBALIANO YA MASHIRIKIANO KATIKA KAZI

   Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri wa Wakala wa Barabara Zanzibar Yasser De Costa amesema ushirikiano wa Wakala wa Barabara Zanzibar na Wakala wa Barabara Tanzania utasaidia kufanya kazi kwa ufanisi.

    Kauli hiyo ameitoa wakati wa utiaji Saini wa makubaliano ya mpango kazi ya utekelezaji kwa Watendaji wa Zanroad na Tanroad huko katika Ofisi za Tanroad Dare-salam na kuwataka Watendaji hao kuhakikisha wanayafuata maelekezo waliyokubaliana ili kufikia lengo.

KIKOSI CHA UTALII NA DIPLOMASIA KUSAIDIA KUKUZA UCHUMI WA NCHI

     Kikosi cha Utalii na Diplomasia wametakiwa  kufuata misingi ya kazi yao  ili  kuendelea kukuza  Maendeleo ya Uchumi wa Nchi kupitia Sekta ya Utalii.

    Waziri wa Utalii na Mambo ya Kale  Mhe Mudrik Ramadhan Soraga ametoa Ushauri huo katika Kikao na Kikosi hicho huko katika Ukumbi wa Idriss Abdulwakil

   Amesema misingi ya kazi ikifuatwa itaimarisha haiba ya utalii hali ambayo itasaidia  kuvutia Watalii wa Ndani na Nje ya Nchi.

Subscribe to Habari
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.