WAZIRI SHARIF AZINDUWA MAANDALIZI YA IJITMAI YA KIMATAIFA KIDOTI

WAZIRI SHARIFF

   Waziri wa Nchi Ofisi ya Raisi  Kazi Uchumi na Uwekezaji Mhe.Sharif Ali Sharif amewataka  Waumini wa Dini ya Kiislam kutoa mali zao na nafsi zao kwaajili ya kupeleka mbele harakati za Kiislam ili kuitengeneza Jamii yenye maadili mema .

    Akizungumza katika Uzinduzi wa harakati za Ijitamia ya Kimataifa ambayo Mwaka huu inatarajiwa kufanyia Kidoti Mkoa wa Kaskazini Unguja Mhe.Sharif amesema  Taasisi za Kidini zina mchango mkubwa katika kuhuisha  maadili mema katika Jamii . 

     Waziri Sharif pia amewasihi  Viongozi wa Jumuiya ya Fisabilahiah  kutumia Ijitmai hiyo  kuwakumbusha Waumini juu ya umuhimu wa kuidumisha amani  na utulivu uliopo  Nchini

     Naibu Mufti Mkuu wa Zanzibar Shekh Mahmoud Mussa Wadi  ameisihi Jamii kufanya mambo ya kheri  ili kupata radhi za Allah   hapa Duniani na Akhera 

     Akizungumza kwa Niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini  Unguja Mkuu wa Wilaya ya Kaskazini 'a' Othman Ali Maulid  amesema Mkoa utaendelea kuunga mkono harakati za kufanikisha  Ijitmai hiyo ikiwemo kuimarisha amani na utulivu .

    Baadhi ya Viongozi wa Jumuiya ya Fisabililah Tabligh Markaz  maiyomba Jamii kuwa mstari wa mbele kushiriki katika harakati mbali mbali na ili kufanikisha Ijitmai hiyo ambayo inatarajiwa kukushanya Waislam kutoka Nchi mbali mbali za Afrika ya Mashairiki ikiwemo Kenya Uganda na Malawi

     Katika Uzinduzi huo ulitanguliwa na Duwa maalum ya kumuombea aliyekuwa Kiongozi wa Jumuiya hiyo Sheikh Said Nyange aliyefariki hivi karibuni huko Saudia Rabia katika Mji Mtukufu wa Makka na Viongozi wengine waliotangilia mbele ya haki.

Tags
stories
standard
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.