MFUMO WA KIELEKRONI MAHAKAMANI WARAHISISHA UENDESHAJI WA KESI

Jaji Mkuu Wa Zanzibar, Khamis Ramadhani Abdalla Amesema Kuwepo Kwa Mfumo Wa Uendeshaji Wa Mashauri Kwa Njia Ya Kielektroniki Kumerahisisha Usikilizaji Wa Kesi, Na Kuchangia Upatikanaji Wa Haki Kwa Haraka.

Akizindua Mfumo Wa Majaribio Wa Uendeshaji Wa Mashauri Kwa Njia Ya Kielektroniki Huko Verde Amesema Lengo La Kuanzisha Mfumo Huo Ni Kuongeza Ufanisi Na Uwajibikaji Katika Mahkama Pamoja Na Kuondosha Urasimu Wa Haki Kwa Wananchi.

WATATU WATHIBITISHWA KUWA WENYEVITI WA BUNGE

Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania leo limewathibitisha Wabunge Deo Mnyika, Cecilia Pareso na Nagma Murtaza Giga kuwa Wenyeviti wa Bunge hilo .

Hayo yamejiri baada ya Spika wa Bunge Mussa Azzan Zungu kuwahoji Wabunge kikanuni kama waanafiki Wabunge hao kuwa Wenyeviti wa Bunge.

Wabunge hao waliteuliwa na Kamati kuu ya Chama cha Mapinduzi CCM kilichoongozwa na Mwenyekiti wa Chama hicho Dkt.Samia Suluhu Hassan January 25 Mwaka huu Mjini Zanzibar.

KILIO CHA SHERIA YA HABARI ZANZIBAR CHAIBULIWA UPYA

Wadau wa Vyombo vya Habari Nchini wameibua tena kilio chao cha kupatikana kwa sheria ya habari hapa Zanzibar na kwa kauli moja wameitaka Wizara ya Habari, Sanaa Utamaduni na Michezo kuhakikisha wanaikata kiu yao ya muda mrefu ya kuipata sheria hii.

Huu ulikuwa ni Mkutano mahususi kati ya Wizara ya Habari, Sanaa Utamaduni na Michezo na Wadau wa Sekta ya Habari ukiwa na lengo la kupata maoni, ushauri kero na mjadala wa kujenga uhuasiano mwema kati ya Sekta ya Habari na Wadau wake.

MAMA SAMIA NI KIONGOZI WA MFANO WA MAENDEELEO

Akinamama waliojifungua katika Hospital ya Wilaya Vitongoji Chake Chake Kituo cha Afya Kendwa na Tundauwa, wamesema Dkt. Samia ni Kiongozi imara na mwenye maono makubwa katika kuileta Nchi maendeleo.

Akinamama hao wameyasema hayo kwa nyakati tofauti mara baada ya kupokea zawadi kutoka  Ofisi ya CCM uratibu Pemba kwa akina mama hao

Waliyojifungua ikiwa ni kusherekea Siku ya Kuzaliwa ya Rais wa Jamuhuri ya Muungano  wa Tanzania Mama Samia Suluhu Hassan .

FUKWE YA FORODHANI SI SALAMA KWA WATOTO KUOGELEA

Kumekuwa na Ongezeko la matukio ya ajali za kuzama kwa Watoto na hata Watu Wazima mara kwa mara katika Eneo la Forodhani. Eneo hilo linatajwa kuwa na kina kirefu cha Maji na hakuna maelekezo ya Tahadhari.

Hapana shaka kwamba Eneo la Forodhani hapa Zanzibar ni moja ya Maeneo yenye Fukwe safi na haiba si tu kustarehe, lakini ile sura ya Utalii wa Zanzibar. hata hivyo baadhi ya Maeneo ya Fukwe hiii maarufu kwa sasa ni hatarishi hususani kwa Watoto kuogelea ama Mtu asiye na ujuzi wa Kuogelea.

UJENZI WA BARABARA TUNGUU-MAKUNDUCHI WAIVA

Asilimia 45 ya Vifaa vitakavyotumika kataika Ujenzi wa Barabara ya Tunguu- Makunduchi na Fumba Kisauni vimekamilika tayari kuanza Ujenzi.

Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Dkt. Khalid Salum Muhamed amekagua Kambi ya Mecco, Kampuni inayojenga Barabara hizo nakueleza kuridhishwa kwake na matayarisho yalifofanyika.

Hii si Biashara ya Gari lakini ni Kambi maalum ya Ujenzi wa Barabara ya Urefu wa Kilomita 48 ya Tunguu-Makunduchi na Barabara ya Fumba Kisauni yenye Urefu wa Kilomita 12.

MKUU WA MKOA WA PWANI, RC KUNENGE ASHIRIKI ZOEZI LA KUPANDA MITI

Katika kusheherekea sikukuu ya kuzaliwa kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan, Mkuu wa Mkoa wa Pwani Alhaji Abubakari  Kunenge ameshiriki zoezi la upandaji wa miti katika shule ya Msingi Chumbi 'A' Wilayani Rufiji Mkoani Pwani.

DKT.SAMIA AWATAKA WATANZANIA KUJENGA UTAMADUNI WA KULINDA MAZINGIRA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan Ametoa wito kwa Watanzania kuendelea kujenga utamaduni wa kulinda na kuhifadhi mazingira kwa hiari wakitambua kuwa ulinzi wa mazingira ni msingi wa uhai, maendeleo na usalama wa Taifa.

Rais Samia ameongoza mchakato wa upandaji miti katika Maeneo ya Bungi kilimo pamoja na Kizimkazi ikiwa ni kuadhimisha Siku yake ya Kuzaliwa ambapo amesisitiza Watanzania kuimarisha uoto wa asili na kuchangia kwa vitendo juhudi za kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabia Nchi kwa ustawi wa Maendeleo ya Taifa.

AJALI YA BASI NA LORI YAUA MMOJA NA KUJERUHI 12 SHINYANGA

Basi la Kampuni ya Kisire limegongana uso kwa uso na lori katika eneo la mnada wa Tinde Wilaya ya Shinyanga na kusababisha kifo cha mtu mmoja huku wengine 12 wakijeruhiwa na kukimbizwa Kituo cha afya Tinde kupata matibabu.

Ajali hiyo imehusisha basi la Kisire lenye namba za usajili T 229 EEL, lililokuwa likitoka Kahama kuelekea Mwanza, kugongana uso kwa uso na lori la mizigo lenye namba za usajili RAE 849N. lililokuwa limebeba shehena ya mchele kutoka Dar es Salaam kwenda nchi jirani ya Rwanda huku chanzo kikielezwa kuwa ni mwendo kasi.

MWENYEKITI RAJABU, TANGA NDIO CHIMBUKO LA SOKA NCHINI

Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Tanga Rajabu Abdallah amesema mkoa huo ndio chimbuko la vilabu vya mpira nchini,hivyo wadau waunge mkono timu za eneo hilo ili kufufua ushindani uliokuwepo.

Akizungumza  wakati wa sherehe za kukabidhi basi kwaajili ya timu ya mpira wa miguu ya African Sports Club zilizofanyika makao makuu ya timu hiyo mwenyekiti Rajabu amesema timu hiyo na Coastal Union ushabiki wake ni zaidia ya Simba na Yanga.

Subscribe to news
 

Simplenews subscription

The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.