MHE. HEMED ATIA SHIME UPATIKANAJI WA DAWA ZA KISUKARI

Makamu Wa Pili Wa Rais Wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla Amesema Serikali Inawajibu Wa Kuweka Mazingira Wezeshi Kupitia Sera Madhubuti, Ufadhili Endelevu Na Ushirikiano Utakao Hakikisha  Changamoto Kubwa Ya Ukosekanaji Wa Dawa Ya Insulini Kwa Watu Wanaoishi Na Ugonjwa Wa Kisukari Inapatiwa Ufumbuzi Wa Haraka.

MADIWANI MBULU WATAKA WASIOCHANGIA CHAKULA SHULENI WACHUKULIWE HATUA

Baraza la madiwani wa halmashauri ya mji wa Mbulu mkoani Manyara wameiomba Serikali  kuwachukulia hatua kali za kisheria Wazazi wasiochangia chakula kwa watoto wao shuleni ili kuwezesha watoto kupata chakula cha mchana na kuinua kiwango cha taaluma.


Madiwani hao Wametoa Ombi hilo wakati wa kikao cha kwanza cha baraza hilo ambapo wamelalamikia tabia ya baadhi ya wazazi kutochangia mchango wa chakula shuleni kwa watoto wao hali inayokuwa kikwazo kwa jitihada za kuinua taaluma na kuondokana na utoro shuleni.

MAHAKAMA YAPENI KIPAUMBELE MASHTAKA YA UKATILI DC KAGANDA.

Serikali Mkoani Manyara imeishauri mahakama kuyapa kipaombele mashauri yanayohusu ukatili wa kijinsia na kutoa adhabu yenye kuleta majuto kwa jamii na wanaohusika na matukio hayo.


Kauli hiyo kwa mahakama Kanda ya Manyara imetolewa na Mkuu wa wilaya ya Babati Emanuela Kaganda kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Manyara Queen Sendiga wakati akizungumza kwenye maadhimisho ya siku ya sheria Nchini yaliyofanyika kwenye viwanja vya mahakama hiyo Mkoani humo.

ZANZIBAR YASAINI MRADI WA KUIMARISHA MIUNDOMBINU

Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imesaini Mkataba wa Miaka Mitano na Czech–Tanzania Development Chamber of Commerce, unaolenga kuimarisha miundombinu na kuchochea uchumi endelevu wa Zanzibar. 

Miongoni mwa Maeneo yatakayotekelezwa ni Sekta ya usafiri wa Anga na Barabara ya Reli na Miradi mingine ya kimkakati ili kuongeza fursa za kiuchumi. 

MAFUNZO YA UTUMISHI KWA WAFANYAKAZI NI MUHIMU KAZINI

Kaimu Mkurugenzi wa Kampuni inayotoa huduma za bima zinazozingatia misingi na sharia ZIC Takaful Ndg.Said Abdallah Basleym amesema suala la Mafunzo kwa Wafanyakazi ni jambo la kupewa kipaumbele ili kuhakikisha wanaendana na kasi ya utendaji na kufanya kazi kwa ufanisi zaidi.

Akizungumza wakati wa Mafunzo ya kujenga uwezo yaliyotolewa kwa Wafanyakazi wa Kampuni hiyo, Ndg. Said ameeleza kuwa uwekezaji katika Mafunzo husaidia kuongeza ufanisi katika utendaji kazi wa Kampuni, pamoja na kuboresha huduma zinazotolewa kwa Wananchi.

MHE. HEMED APONGEZA MCHANGO WA TAASISI ZA DINI KUSIMAMIA MAADILI

Makamu Wa Pili Wa Rais Wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdullah Amesema Serikali Inatambua Na Kuthamini Mchango Wa Viongozi Wa Dini Katika Kuimarisha Amani, Maendeleo Na Maadili Mema Kupitia Mafundishoya Dini.

Mh. Hemed Suleiman Ametoa Kauli Hiyo Wakati Akizungumza Katika Uzinduzi Wa Mashindano Ya Qur’an Ya Mabara Yote Ulimwenguni Yanayo Ratibiwa Na Taasisi Ya Al Hikma Jijini Dar Es Salaam

Huku Akiwasihi Wanamchi Kuendelea Kushikamana Katika Kulinda Na Kutunza Amani Ya Nchi.

TANESCO LINDI YAWANASA WATU WAWILI KWA KUJIUNGANISHIA UMEME KINYUME CHA SHERIA

Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Mkoa wa Lindi limeendesha oparesheni maalumu ya kudhibiti vitendo vya kujiunganishia umeme kiholela na kinyume cha sheria, ambapo limefanikiwa kuwakamata watu wawili wanaodaiwa kujiunganishia huduma hiyo bila kufuata taratibu.

FURSA MPYA KWA VIJANA BILIONI 2 KWA WATENGENEZAJI WA MAUDHUI

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Paul Makonda, amesema Wizara imepatiwa kiasi cha TZS bilioni 2 itakayowawezesha watengenezaji wa maudhui mbalimbali mitandaoni kuimarisha kazi zao na kuwaongezea kipato kupitia majukwaa ya kidijitali.

Amesema hayo Januari 29, 2026 jijini Dodoma na kubainisha kuwa, fedha hizo zimetolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa lengo la kuyawezesha makundi yote ya watengeneza maudhui ikiwemo katika Sekta ya Utalii, Michezo, Habari, Jamii, Muziki, Filamu na sanaa nyinginezo.

SHETTA AIWAKILISHA DAR ES SALAAM KATIKA JUKWAA LA UONGOZI WA MAMEYA AFRIKA

Mstahiki Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Nurdin Bilal Juma (Shetta), kwa sasa yupo Cape Town, Afrika Kusini, akishiriki katika mkutano wa African Mayoral Leadership Initiative (AMALI) unaowakutanisha mameya na viongozi wa miji kutoka barani Afrika.

Katika mkutano huo, Mstahiki Meya alipata fursa ya kuwasilisha maono ya urithi wa uongozi (legacy pitch) kwa niaba ya Jiji la Dar es Salaam akiweka mbele ajenda ya maendeleo jumuishi, ajira kwa vijana, na uongozi wa miji unaozingatia watu.

DKT SAMIA AZINDUA MPANGO WA KUSOMA KUANDIKA NA KUHESABU

Rais Wa Jamuhuri Ya Muungano Wa Tanzania Mh.Dk. Samia Suluhu Hassan Amezindua Mpango Mkakati Wa Sayansi Wa Kujenga Umahiri Wa Kusoma, Kuandika Na Kuhesabu (Kkk)Kwa Watoto Wa Elimu Awali Na Wanafunzi Wa Darasa La Kwanza Na La Pili.

Akizungumza Katika Uzinduzi Wa Mpango Huo Uliofanyika Jiji Dar Es Salaam, Rais SamiaAmesema Kuwa Serikali Imejidhadhati Kuhakikisha Kuwa Hakuna Mtoto Atakaye Fika Darasa La Tatu Bila Ya Kuwa Na Uwezo Wa Kusoma Kuandika, Kuandika Na Kuhesabu. 

Subscribe to news
 

Simplenews subscription

The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.