DKT. SAMIA AWAHIMIZA WATENDAJI KUWAJIBIKA

Raisi Wa Jamhuri Ya Muungano Wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan Amewaapisha Viongozi Aliowateua Hivi Karibuni Na Kuwataka Kuwajibika Ipasavyo Ili Kufanikisha Utekelezaji Wa Dira Ya Taifa.

Hafla Hiyo Ya Uapisho Iliyofanyika Ikulu Ya Magogoni Jijini Dar Es Salaam, Iliwahusisha Wakuu Wa Mikoa, Makatibu Wakuu, Makatibu Tawala Wa Mikoa, Naibu Makatibu Wakuu, Katibu Mtendaji Wa Tume Ya Mipango, Naibu Katibu Mtendaji Wa Tume Ya Mipango, Na Balozi Iliambatana Na Kiapo Cha Ahadi Ya Uadilifu Wa Watumishi Wa Umma.

TAASSI ZA ELIMU ZASISITIZWA KUWEKEZA KWENYE UTAFITI

Wito Umetolewa Kwa Taasisi Binafsi Kushirikiana Vyema Na Taasisi Za Elimu Pamoja Na Kuekeza Katika Tafiti Hususan Za Kisayansi Na Teknolojia Kuhimiza Ubunifu Katika Ufundishaji Na Ujifunzaji Ili Kuinua Viwango Vya Tafiti Na Ubora Wa Elimu.

Wito Huo Umetolewa Jijini Dar Es Salaam Na Makamu Wa Rais Wa

SMZ YAWEKEZA ZAIDI YA SH. BIL. 13 KATIKA MAHAKAMA

Serikali Ya Mapinduzi Ya Zanzibar Imechukua Hatua Thabiti Ya Kuweka Mazingira Bora Ya Kufanyia Kazi Kwa Mhimili Wa Mahakama.

Amesema Katika Mwaka Wa Fedha 2025/2026 Serikali Imewekeza Zaidi Ya Fedha Za Kitanzania Shilingi Bilioni 13.6 Kwa Ajili Ya Ujenzi Wa Majengo Ya Kisasa Ya Mahakama Ambayo Yanaendana Na Uwekaji Wa Miundombinu Ya Tehama.

Baada Ya Shamrashamra Ya Wiki Ya Sheria, Hatimae Kilele Cha Maadhimisho Hayo Yamefanyika Kisiwani Pemba.

WAZIRI MKUU ACHUKIZWA NA MIGOGORO YA ARDHI

WAZIRI MKUU, Dkt. Mwigulu Nchemba amewasisitiza Mawaziri, Wakuu wa Mikoa, Wakuu wa Wilaya pamoja na watumishi wa umma wahakikishe wanatenga muda wa kusikiliza na kutatua kero za wananchi katika maeneo yao hususani kwenye migogoro ya ardhi katika ngazi zao za kiutawala. 
 
Ameyasema hayo leo Ijumaa, Februari 6, 2026 wakati wa kuahirisha Mkutano wa Pili wa Bunge la 13 jijini Dodoma, akisisitiza kuwa viongozi hao wanapaswa kuwafuata wananchi, kuwasikiliza na kuchukua hatua za haraka za kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili wakiwa katika maeneo yao.

DKT. MWINYI KUFUNGUA IJTIMAI ZANZIBAR

Rais Wa Zanzibar Na Mwenyekiti Wa Baraza La Mapinduzi, Alhaj Dkt. Hussein Ali Mwinyi, Kesho Anatarajiwa Kuwa Mgeni Rasmi Katika Ufunguzi Wa Ijtimai Ya Kimataifa Itakayofanyika Katika Eneo La Fuoni Migombani.

Maandalizi Ya Ijitimai Hiyo Tayari Yamekamili Huku Waumini Wa Dini Ya Kiislamu Wakihimizwa Kuhudhuria Katika Ijitimai Hiyo Ambayo Itawakumbusha Mambo Ya Heri Na Kumcha Mwenyezi Mungu.

WADAU WA USALAMA BARABARANI WATAKIWA KUSHIRIKIANA

Mkuu Wa Mkoa Wa Mjini Magharibi, Moh’d Abdalla Ali, Amesema Wafanyabiashara Wa Soko La Mombasa Wanatarajiwa Kuanza Kufanya Biashara Zao Ndani Ya Soko Hilo Katika Kipindi Cha Hivi Karibuni.

Akizungumza Na Waandishi Wa Habari, Mheshimiwa Mohd Abdalla Ali Amesema Tayari Wameshagawa Vizimba Kwa  Wafanya Biashara Na Wanatarajia Kuanza Kulitumia Soko  Kabla Ya Mwezi Wa Ramadhani

ZBC YATUNUKU ZAWADI KWA WAFANYAKAZI BORA

Mwenyekiti Wa Bodi Ya Shirika La Utangazaji Zanzibar Zbc Mhandisi Idrisa Muslim Hijja Amesema Ili Kufikia Dhamira Ya Serikali Kuimarisha  Maendeleo Ni Muhimu Kwa Wafanyakazi Kujituma Zaidi Katika Kutekeleza Majukumu Yao

 

Akizungumza Katika Hafla Ya Kuwapongeza Wafanyakazi Wa Shirika Za Utangazaji Zbc Waliofanya Vizuri Kwa Mwaka Huu Kupitia Hafla Maalum Ya Utoaji Tuzo Amesema Hatua Inalenga Kuimarisha Uwajibikaji ,Ubunifu Na Kuongeza Motisha Katika Kufanya Kazi

KATIBU NEC ATEMBELEA MIRADI YA AFYA HOSPITALI YA RUFAA KILIMANJARO

Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) wa Siasa na Uhusiano wa Kimataifa (SUKI), Rabia Abdalah, ambaye pia ni mlezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoani Kilimanjaro, ametembelea Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Kilimanjaro kwa lengo la kujionea utekelezaji wa baadhi ya miradi ya maendeleo inayoendelea katika hospitali hiyo.

ACT WAZALENDO YAIOMBA ZEC KUSIMAMISHA UCHOMAJI NYARAKA ZA UCHAGUZI

Chama cha ACT Wazalendo Zanzibar kimeiomba Tume ya Uchaguzi Zanzibar–ZEC kusimamisha zoezi la uteketezaji wa nyaraka na vifaa vya Uchaguzi kwa kile walichodai ni mpaka mashauri yaliyoko Mahakamani yamalizike.

Kauli hii imekuja kutokana na Tamko la Tume ya Uchaguzi lililotolewa hapo Jana likieleza nia ya Tume kuteketeza nyaraka zote za Uchaguzi wa Mwaka 2025 kwa baada ya Siku 90 kwa mujibu wa Sheria.

UWEKEZAJI ZANA ZA KILIMO AFRIKA HAIENDANI NA MAHITAJI HALISI

Tanzania Kwa Kushirikiana Na Shirika La Kilimo Na Chakula La Umoja Wa Mataifa (Fao) Imeandaa Mkakati Wa Taifa Wa Zana Za Kilimo Unaolenga Kuimarisha Matumizi Ya Uzalishaji, Usimamizi Na Uratibu Wa Teknolojia Za Kilimo.

Subscribe to news
 

Simplenews subscription

The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.