Rais Wa Zanzibar Na Mwenyekiti Wa Baraza La Mapinduzi, Alhaj Dkt. Hussein Ali Mwinyi, Kesho Anatarajiwa Kuwa Mgeni Rasmi Katika Ufunguzi Wa Ijtimai Ya Kimataifa Itakayofanyika Katika Eneo La Fuoni Migombani.
Maandalizi Ya Ijitimai Hiyo Tayari Yamekamili Huku Waumini Wa Dini Ya Kiislamu Wakihimizwa Kuhudhuria Katika Ijitimai Hiyo Ambayo Itawakumbusha Mambo Ya Heri Na Kumcha Mwenyezi Mungu.
Katibu Wa Jumuiya Ya Faysabillah Tabligh Markaz, Amir Kassim Saleh Abdallah, Amesema Maandalizi Ya Ijtimai Hiyo Yanaendelea Vizuri Na Kuwaomba Waumini Kujitokeza Kwa Wingi Kushiriki Katika Tukio Hilo Muhimu La Kidini.
Aidha, Amesema Kuwa Wageni Kutoka Nchi Mbalimbali Tayari Wamewasili, Wakiwemo Kutoka Nairobi Na Mombasa Nchini Kenya, Pamoja Na Wageni Kutoka Mikoa Mbalimbali Ya Tanzania Bara.
Wakizungumza Wakati Walipowasili Katika Eneo La Fuoni Linalotarajiwa Kufanyika Ijitimai Hiyo , Waumini Kutoka Mombasa, Nairobi Na Tanzania Bara Wamesema Wamekuwa Wakishiriki Katika Ijtimai Za Zanzibar Kila Mwaka, Kutokana Na Mapokezi Mazuri Wanayopata Katika Kulitangaza Jina Tukufu La Mwenyezi Mungu.
