ZBC YATUNUKU ZAWADI KWA WAFANYAKAZI BORA

MKURUGENZI SHIRIKA LA UTANGAZAJI ZANZIBAR  ZBC
English

Mwenyekiti Wa Bodi Ya Shirika La Utangazaji Zanzibar Zbc Mhandisi Idrisa Muslim Hijja Amesema Ili Kufikia Dhamira Ya Serikali Kuimarisha  Maendeleo Ni Muhimu Kwa Wafanyakazi Kujituma Zaidi Katika Kutekeleza Majukumu Yao

 

Akizungumza Katika Hafla Ya Kuwapongeza Wafanyakazi Wa Shirika Za Utangazaji Zbc Waliofanya Vizuri Kwa Mwaka Huu Kupitia Hafla Maalum Ya Utoaji Tuzo Amesema Hatua Inalenga Kuimarisha Uwajibikaji ,Ubunifu Na Kuongeza Motisha Katika Kufanya Kazi

Mwenyekiti Wa Bodi Mhandisi Idrisa Amesema Shirika La Utangazaji Limepiga Hatua Kubwa Kwa Kufikia Mafanikio Hivyo Wafanyakazi Wanapaswa Kuongeza Juhudi Maarifa Na Kujituma Ili Kufanikisha Maendeleo Ya Nchi

Mkurugenzi Mkuu Shirika La Utangazaji Zanzibar Ramadhan Bukini Amesema Utoaji Wa Tuzo Hizo Ni Sehemu Ya Kutambua Mchango Wa Wafanyakazi Waliofanya Vizuri Zaidi Na Amesema Zoezi Hilo La Ugawaji Wa Tuzo Ni Endelevu 

Baadhi Ya Washindi Wa Tuzo Hizo Wamesema Kutambuliwa Kwao Kumewapa Nguvu Ya Kuendelea Kufanya Kazi Kwa Juhudi Na Nidhamu Na Wakiahidi Kuendeleza Viwango Vya Juu Vya Utendaji

 

Simplenews subscription

The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.