VYOMBO VYA ULINZI VIMETAKIWA KUTEKELEZA MAJUKUMU YAO KIKATIBA

Makamu Wa Pili Wa Rais Wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla Amesema Msingi Mkubwa Ya Wiazara Ya Mambo Ya Ndani Ya Nchi Ni Kuhakikisha Inalinda Wananchi Na Mali Zao Pamoja Na Kutenda Haki Kwa Raia Wa Jamuhuri Ya Muungano Wa Tanzania.

Akizungumza Na Uongozi Wa Wizara Ya Mambo Ya Ndani Ya Nchi Uliofika Ofisini Kwake Baraza La Wawakilishi Chukwani Zanzibar Kwa Ajili Ya Kujitambulisha Amesema Suala La Usalama Wa Raia Na Mali Zao Ni Muhimu  Katika Kuimarisha Nchi Kisiasa,  Kiuchumi Na Kijamii 

KISWAHILI CHATAMBULIWA KIMATAIFA

Katibu Mtendaji Wa Kamisheni Ya Kiswahili Afrika Mashariki, Dkt. Caroline Asiimwe, Amesema Kiswahili Kimepiga Hatua Kubwa Kimataifa, Kikitambuliwa Na Umoja Wa Mataifa Na Unesco Kama Lugha Yenye Mchango Muhimu Duniani.

Hatua Hiyo Inatokana Na Idadi Ya Wanaozungumza Ikiendelea Kuongezeka Barani Afrika Na Kutumika Katika Majukwaa Ya Kidiplomasia, Biashara Na Teknolojia Jambo Linalothibitisha Kuwa Si Lugha Ya Kikanda Pekee, Bali Ni Sauti Ya Afrika Katika Jukwaa La Dunia.

ZAA YAKANUSHA TAARIFA ZA WIZI WA MIZIGO UWANJA WA NDEGE WA (AAKIA)

Zanzibar, 11 Februari 2026 Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Zanzibar (ZAA), Ndugu Seif Abdalla Juma, ametoa ufafanuzi kwa umma kufuatia taarifa zilizosambazwa kwenye baadhi ya mitandao ya kijamii na vyombo vya habari zikidai kuwa mamlaka hiyo imeshindwa kudhibiti matukio ya wizi wa mizigo katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume (AAKIA).

WAZIRI MKUU DKT. MWIGULU NCHEMBA AFUNGUA UWANJA WA NDEGE WA MTEMERE

Waziri Mkuu Dkt. Mwigulu Nchemba leo Februari 11, 2026 amezindua uwanja wa ndege Mtemere uliopo katika kijiji cha Mloka, mkoani Pwani kwenye hifadhi ya Taifa ya Nyerere.

Uzinduzi wa uwanja huo umeenda sambamba na uzinduzi wa miradi mingine 20 (kufanya miradi 21) ikiwemo Malango ya kuingilia Hifadhini, vituo vya taarifa kwa wageni, kambi za wageni, Eneo la Kupumzikia wageni, Nyumba za wageni, Hosteli za Wanafunzi, kituo cha kufuatilia ikolojia, na vituo vya askari.

JAPAN NA ZANZIBAR ZAAHIDI KUSHIRIKIANA

Makamu Wa Pili Wa Rais Wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla Amesema Serikali Ya Mapinduzi Ya Zanzibar Itaendeleza Uhusiano Ulipo Kati Ya Serikali Ya Japan Na Zanzibar Uliodumu Kwa Muda Mrefu.

Mhe. Hemed Ameyasema Hayo Alipofanya Mazungumzo Na Balozi Wa Japan Nchini Tanzania Yoichi Mikami Afisini Kwake Vuga Zanzibar.

Amesema Uhusiano Uliopo Kati Ya Tanzania Na Japan Utaendelea Kukuza Ushirikiano Katika Pande Zote Mbili Katika Kuimarisha Sekta Za Kilimo, Biashara, Maji Safi Na Salama, Maendeleo Ya Viwanda, Utalii Na Miundombinu Mbali Mbali.

SEKTA YA FEDHA NGUZO YA UCHUMI ENDELEVU

Waziri Wa Fedha Na Mipango Dkt. Malik Akili Amesema Sekta Ya Fedha Ni Moja Ya Eneo Litakalofanya Uchumi Wa Zanzibar Kuwa Endelevu Kama Ilivyoainishwa Katika Dira Ya Maendeleo Ya 2050.

Dkt. Malik Ameyasema Hayo Katika Ufunguzi Wa Tawi La Benki Kcb Mkunazini Zanzibar.

Katika Ufunguzi Wa Benki Hiyo, Dkt. Malik Amesema Sera Hiyo Inalenga Kuwepo Na Mageuzi Ya Kiuchumi Kwa Kuhakikisha Watu Wote Wanajumuishwa Katika Masuala Ya Kifedha Ikiwemo Huduma Za Kibenki.

NDANI YA SIKU 100 WIZARA TUMEFANIKIWA KUTOA AJIRA 2,300

Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya Zanzibar, Dkt. Mngereza Mzee Miraji, ameeleza utekelezaji wa majukumu ya Wizara ya Afya kuanzia ngazi ya msingi hadi ngazi ya juu ya rufaa, ikiwa ni sehemu ya kuimarisha mfumo wa huduma za afya Zanzibar.

Ndani ya siku 100 za utekelezaji, Wizara imefanikiwa kuajiri wahudumu wa afya ngazi ya jamii 2,300, hatua iliyopanua upatikanaji wa huduma za afya mashinani, sambamba na kuhakikisha mishahara inalipwa kwa wakati kutokana na uongozi na maelekezo ya Mheshimiwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi.

SMZ IMEFANYA MAPINDUZI MAKUBWA KWENYE SEKTA YA AFYA

Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya Zanzibar, Dkt. Mngereza Mzee Miraji, ameeleza kwa kina dira ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi, ya kuiondoa Zanzibar katika utegemezi wa rufaa za matibabu nje ya nchi na badala yake kuijenga kuwa kitovu muhimu cha huduma za afya katika ukanda wa Afrika Mashariki.

ZANZIBAR INAENDELEA KUPIGA HATUA KWENYE SEKTA YA UTALII KIMATAIFA

Katibu Mkuu wa Wizara ya Utalii na Mambo ya Kale, Dkt. Aboud Suleiman Jumbe Akizungumza katika tathmini ya utekelezaji wa siku 100, amesema Zanzibar imeendelea kufanya vizuri na kujipatia nafasi kwenye orodha mbalimbali za kimataifa za utalii.

Ameeleza kuwa Zanzibar sasa ipo katika kumi bora barani Afrika kwenye vivutio vya utalii, miradi bora ya kitalii, maeneo bora ya honeymoon pamoja na michezo ya baharini, hali inayoongeza ushindani na kuimarisha nafasi ya Zanzibar katika soko la kimataifa la utalii.

ZANZIBAR SEKTA YA UTALII INAKUA KWA KASI, ZAIDI YA WATALII LAKI 1 WANATEMBELEA KWA MWEZI

Baada ya kuapishwa kwa Mhe. Rais  Dkt. Hussein Mwinyi kuongoza Zanzibar katika awamu ya nane ya uongozi, sekta ya utalii imeonesha ukuaji mkubwa na wa kasi. Katika mwezi wa kwanza wa uongozi huo, idadi ya watalii ilikuwa takribani elfu 72 pekee.
Hata hivyo, kwa sasa kuanzia Novemba hadi Januari, Zanzibar inapokea wastani wa watalii laki 1 kwa kila mwezi.

Subscribe to news
 

Simplenews subscription

The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.