RC TANGA ATOA AGIZO KWA WAKUU WA WILAYA KUHUSU WAMACHINGA

Mkuu wa mkoa wa Tanga Balozi Batilda Buriani amewaagiza wakuu wa wilaya zote za eneo hilo kuwatafutia maeneo ya uhakika wafanyabiashara ndogondogo maarufu kama Machinga,na katafuta sehemu ambayo watakaa bila changamoto

Akizungumza wakati akifunga maadhimisho ya wiki ya huduma za fedha kitaifa yaliofanyika mkoani Tanga katika viwanja vya shule ya sekondari usagara kwa wiki moja Jumatatu Januari 26,2026 Balozi Batilda amesema wafanyabiashara ndogondogo wanatakiwa kuwekwa sehemu  nzuri.

HATUJAANGUSHA NDEGE NI ZOEZI LA UTAYARI (ZAA)

Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Zanzibar (ZAA) imefanya zoezi la utayari ikiwa ni sehemu ya majukumu yake ya kawaida ya usalama wa anga katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume (AAKIA), lenye lengo la kupima uwezo wa kukabiliana na matukio ya dharura yanayoweza kutokea katika Viwanja vya Ndege.

NGUVU YA PAMOJA INAHITAJIKA KUKOMESHA UKATILI WA KIJINSIA

Nairat Abdallah Ali ndie Mkurugenzi mpya wa Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake TAMWA Zanzibar 

Nairat anachukuwa nafasi hiyo kutoka kwa Dkt. Mzuri Issa aliyehudumu katika nafasi hiyo kwa Kipindi cha Miaka 19

 

 

ZANZIBAR YAJIANDAA NA DHARURA ZA NDEGE

Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Zanzibar imefanikiwa kutekeleza zoezi la kujiandaa na kukabiliana na dharura za Ndege, hatua inayolenga kuimarisha uratibu kati ya Taasisi za Ulinzi, usalama na usimamizi wa maafa.  Zoezi hilo limefanyika katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa Abeid Amani Karume 

Hayo yamebainishwa na Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Zanzibar Mulhat Yussuf Said wakati akizungumza na Waandishi wa Haaabari 

TUME YA TAIFA YA MIPANGO YA MATUMIZI YA ARDHI YATATUA MGOGORO ULIODUMU MIAKA 10 WILAYA YA KISARAWE

Tume ya Taifa ya Mipango ya Matumizi ya Ardhi (NLUPC) imefanikiwa kutatua mgogoro  wa mpaka  kati ya vijiji viwili uliyodumu zaidi ya  miaka kumi huko Wilaya Kisarawe Mkoani Pwani.

SERIKALI YASAINI MKATABA UJENZI HOSPITALI YA MKOA MAHONDA

 Wizara ya Afya Zanzibar imetiliana Saini Mkataba wa Ujenzi wa Hospital ya Mkoa Mahonda na Kampuni Cross World Construction Limited.

Akizungumza baada ya Utaji Saini Mkataba huo Kaimu Waziri wa Afya Zanzibar Dkt. Saada Mkuya Salum amesema Mradi huo utakua ufumbuzi wa upatikanaji wa huduma za Kibingwa za Afya na kuipunguzia gharama Serikali ya kusafirisha Wagonjwa kutoka Nje ya Nchi.

HISTORIA YAANDIKWA MABASI YA UMEME YAWASILI ZANZIBAR

Zanzibar imeandika historia Barani Afrika baada ya kuingiza Mabasi ya Umeme kwa mara ya kwanza. Serikali kupitia mradi wa usafiri wa kisasa imepokea Mabasi Kumi ya Umeme, ikiwa ni hatua ya Mwanzo ya mpango wa kuingiza Jumla ya Mabasi Mia Moja. 

Mabasi hayo yanatarajiwa kuanza kufanya kazi rasmi Mwezi wa Tatu baada ya kukamilika kwa taratibu na Sheria husika. hatua hii inalenga kuboresha Usafiri wa Umma na kupunguza uchafuzi wa Mazingira.

TANZANIA KUENDELEA KUSHIRIKIANA NA NCHI ZA NODIKI KATIKA SEKTA YA AFYA

Ubalozi wa Tanzania nchini Sweden umeratibu ushiriki wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika uzinduzi wa Mkutano wa Afya kati ya nchi za Nodiki na Afrika uliofanyika tarehe 22 Januari, 2026, jijini Stockholm, Sweden, ili kujadiliana masuala ya afya ya uzazi na mtoto na mapambano dhidi ya magonjwa yasiyoambukiza.
 

BULGARIA AIR YAANZA RASMI SAFARI ZAKE ZANZIBAR

Mapokezi ya Shirika la Ndege la Bulgaria Air (Bul Air) katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume (AAKIA)  Alhamis ya Tarehe 22 Januari 2026

Ndege Aina ya Airbus a 320 iliwasili Uwanjani hapo Majira ya saa 5:30 Asubuhi ikitokea Jijini Sofia ikiwa na Jumla ya Abiria 180.

Shirika hilo la Ndege sasa limeanza rasmi safari zake na linatarajiwa kuwasili Zanzibar MaraTatu kwa Mwezi.

WAZIRI MKUU DKT. MWIGULU NCHEMBA AWEKA JIWE LA MSINGI MRADI WA KUSUKUMA NA KUHIFADHI MAJI MWANZA

Waziri Mkuu, Dkt. Mwigulu Nchemba, ameweka jiwe la msingi la Mradi wa Ujenzi wa Miundombinu ya Kusukuma na Kuhifadhi Maji katika mkoa wa Mwanza, mradi unaolenga kuboresha usambazaji wa maji safi na salama kwa wananchi.

Subscribe to news
 

Simplenews subscription

The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.