Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan Ametoa wito kwa Watanzania kuendelea kujenga utamaduni wa kulinda na kuhifadhi mazingira kwa hiari wakitambua kuwa ulinzi wa mazingira ni msingi wa uhai, maendeleo na usalama wa Taifa.
Rais Samia ameongoza mchakato wa upandaji miti katika Maeneo ya Bungi kilimo pamoja na Kizimkazi ikiwa ni kuadhimisha Siku yake ya Kuzaliwa ambapo amesisitiza Watanzania kuimarisha uoto wa asili na kuchangia kwa vitendo juhudi za kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabia Nchi kwa ustawi wa Maendeleo ya Taifa.
Rais Dkt.Samia ameielekeza Wizara ya Ardhi kuhakikisha wanatenga Maeneo ili kupanda Miti na kuendeleza Kijani endelevu.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhandisi Hamad Yussuf Masauni amesema maelezo ya Dkt.Samia yanatekelezwa ipasavyo kwa kusimamia mpango wa nishati safi Nchini .
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Sera Uratibu na Baraza la Wawakilishi Mhe Hamza Hassan Juma amesema hatua hiyo ni chachu ya kuleta mabadiliko katika Jamii.
Mkuu wa Mkoa Kusini Unguja Hamida Khamis Mussa baada ya kutoa salamu za Mkoa huo akataja Idadi ya Miti iliyopandwa kuwa ni 1705 ikiwemo ya Matunda 105 na Misitu 1600.
Tarehe 27 ya Kijani na Mti wa Mama inaongozwa na kaulimbiu "UZALENDO NI KUTUNZA MAZINGIRA ,SHIRIKI KUPANDA MITI "




