WATENDAJI WA TAKWIMU KWENDANA NA MABADILIKO YA TEKNOLOGIA .

NAIBU WAZIRI FEDHA

Miundombinu ya kisasa ya matumizi ya Teknolojia  ni msingi muhimu wa kuimarisha Ufanisi wa shughuli za Kitakwimu kwa njia ya usahihi  na uwezo wa kuchambua data kwa haraka na kutoa Taarifa zenye ubora wa hali ya juu.

Akizungumza katika Uzinduzi wa Mradi  wa kuwajengea uwezo Watakwiku katika mifumo wa Teknologia Naibu Waziri  wa Fedha na mipango Mh Juma Makungu Juma  amesema matumizi ya Teknologia  katika mifumo ya Kitakwimu yatawawezesha watakwimu kutoa Takwimu bora jambo litakaloiwezesha Serikali   kupanga  sera na mipango endelevu kwa  Maendeleo ya Taifa .

Mtakwimu Mkuu wa Serikali Salum Kassim Ali amewataka Watendaji hao kuyafanyia kazi mafunzo waliyoyapata ili kuleta mabadiliko ya kiutendaji na kuongeza wigo wa utowaji wa Takwimu kisasa na kuachana na Mifumo ya kizamani.

Mradi huo  wa  kuwajengea uwezo Watakwimu katika mifumo wa Teknologia  ni wa Miaka miwili  na unatekelezwa na Ofisi ya mtakwimu Mkuu Serikali zanzibar kwa kushirikiana na Serikali ya Korea ya Kusini 

stories
standard
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.