Waislamu wa Maeneo Mbalimbali Zanzibar wamejitokeza katika Matembezi ya maadhimisho ya Mwaka Mpya wa Kiislamu huku Viwanja vya Mnazi Mmoja.
Akipokea Matembezi ya Mwaka Mpya wa Kiislam Spika wa Baraza la Wawakilishi Mhe.Zuberi Ali Maulid amesema Maadhimisho hayo yanakumbusha Safari ya Mtume wakati alipohama Makka kuelekea Madina hivyo Waumini wa Kiislamu na Watu wengine wana mengi ya kujifunza katika kutekeleza maamrisho ya Mwenyezi Mungu.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Katiba Sheria Utumishi na Utawala Bora Mhe.Haroun Ali Suleiman amesema hatua hiyo ni alama inayoonesha Zanzibar katika kutekeleza maamrisho ya Dini kivitendo Jambo ambalo linafundisho kwa Mataifa mengine Duniani.
Mwenyekiti wa Zafa Shekha Abdulrahman Sheikh Alhabash na Mkuu wa Baraza la Maulamaa Zanzibar Shekh Samir Zulfikar wamesema maadhimisho hayo yanashajihisha Waislamu kuitambua vyema Dini yao