Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango ameiagiza Wizara ya Ujenzi kuhakikisha inakamilisha Ujenzi wa Barabara kwa kiwango cha Lami Malagarasi – Uvinza ifikapo Mwezi Machi 2025 kama ilivyopangwa.
Makamu wa Rais ametoa maelekezo hayo mara baada ya kukagua maendeleo ya Ujenzi wa Barabara hiyo akiwa Ziara Mkoani Kigoma.
Amewasihi Viongozi na Watendaji kuhakikisha Wanasimamia Barabara hiyo ili iweze kukamilika kwa wakati na kuwawezesha Wananchi kushiriki vema shughuli za Kiuchumi na Ujenzi wa Taifa.
Makamu wa Rais amewasihi Watendaji wa Wizara ya Ujenzi pamoja na Mkandarasi kutumia vyema Msimu huu wa Kiangazi kuhakikisha wanafanyakazi kwa haraka bila kupoteza ubora unaotarajiwa ili Barabara hiyo iwezekukamilika kabla ya ujio wa mvua.
Katika hatua nyingine Makamu wa Rais amekagua maendeleo ya Ujenzi wakituo cha kupooza Umeme wa msongo wa kv 132 kilichopo Kijiji cha Ngurukawilaya ya Uvinza mkoani Kigoma ambapo ameipongeza wizara yanishati kwa Maendeleo ya Ujenzi wa kituo hicho ambacho kimefikia asilimia95.
Aidha Makamu wa Rais ameuagiza Uongozi wa Mkoa wa kigoma kufuatilia haraka Tatizo la Mifugo hasa Ng’ombe kutawanywa ovyo na kula Mazao ya Wakulima katika Wilaya ya Uvinza.