Waziri wa Viwanda na Biashara, Dkt. Selemani Jafo hakurizishwa na kiwango cha Watanzania kutumia Mbolea ya kiwanda ya cha Intracom kilichopo nala Jijini Dodoma.
Akizungumza na Waandishi wa Habari mara baada ya kufanya Ziara kwenye kiwanda hicho, Waziri Jafo amesema kuwa kina uwezo wa kuzalisha Tani Milioni moja kwa Mwaka na mahitaji ya mbolea kwa mujibu wa Wizara ya Kilimo ni Tani 700,000 na kwamba Kiwango kilichozalishwa kwasasa Takwimu zinaonesha kiwango kidogo kimeuzwa Nchini.
Katika hatua nyingine Waziri Jafo jafo amekagua Ujenzi wa jengo la Wizara hiyo katika Mji wa Serikali Mtumba Jijini Dodoma na kuwataka Wakandarasi kuhakikisha wanakamilisha kwa wakati.
Naye, Mkurugenzi wa Kiufundi wa Kiwanda cha Intracom , Mhandisi Victor Ngendazi,amesema wamekuwa wakishirikiana na Serikali ya Tanzania kutatua changamoto zilizokuwapo zikiwakabili na kusisitiza uwezo wa uzalishaji upo wa kutosha.