Bodi ya usajili, Wasinifu, Wahandisi na Wakadiriaji majengo Zanzibar imewataka Wataalamu kufuata sheria na kanuni zinazowaongoza ili kuweza kujisajili kwa Lengo la kufanyakazi zao kwa Ubunifu na ufanisi kwa mslahi ya Wananchi na Taifa.
Akizungumza mara baada ya kutembelea Miradi tofauti ya Ujenzi . Mkoa wa Kaskazini Pemba ;Mwenyekiti wa Bodi hiyo Yasser De Costa amesema kwa mujibu wa Sheria ya Bodi hiyo Namba 5 ya Mwaka 2008 ni kosa Kisheria kwa Wataalamu hao kufanya kazi Ikiwa bado hawajajisajili .hivyo bodi hiyo itahakikisha inasimamia na kufuatilia ili Wataaluma hao waweze kujisajili kwa lengo la kuwa na majengo madhubuti kwa Maslahi ya Wananchi na Taifa.
Nae Mrajisi wa Bodi hiyo Mhandisi Mansour rashid amesema wamefafanya Ziara ya Hiyo ili kujua Miradi inayotekelzwa ambayo haijasajili pamoja na Wataalamu wake ili Kuweza kuwachua hatua za Kisheria.
Mkandarasi wa Skuli ya msingi Kojani Hawa Natepe amesema wanakabiliwa na Changamoto kadhaa katika Miradi ya Ujenzi Visiwani ikiwemo usafirishaji wa Vifaa.
Akitowa Shukrani zake kwa bodi hiyo pamoja na Serikali kwa kufanikisha Ujenzi wa Skuli ya Msingi ya Horofa katika eneo lao Shekhe Suleiman Salim Hamad Mkaazi wa Kojani amesema wamefarijika kuona Kisiwa chao ni Miongoni mwa maeneo Yanayoendelea kufaidika na juhudi za Serikali .