Akizungumza katika Maadhimisho ya Siku ya Mapambano dhidi ya Rushwa Afrika yaliyofanyika katika Ukumbi wa Kimataifa wa Maonenyesho Nyamanzi Dkt.Mwinyi amesema Mapambano dhidi ya Rushwa na Uhujumu Uchumi ni miongoni mwa vipaumbele vya Serikali katika kuandaa mipango madhubuti itakayosaidia kuokoa hali ya Uchumi wa Nchi .
Amesema katika kufanikisha hilo Serikali inameanza kutumia sheria ya kumlinda mtoa Taarifa za Rushwa na Uhujumu Uchumi dhidi ya mtuhumiwa ambayo hatua hiyo itamsaidia kumpa ulizi na usalama wa Maisha yake
Mkurugenzi Mkuu wa ZAECA Ali Abdallah Ali na Naibu Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU Neema Mwakalile wamesema wataendelea kushirikiana kufuatilia vyanzo vya Miradi ya Maendeleo pamoja na Maeneo ya Rushwa ili hali hiyo isiendelee kufanyika.
Katika Maadhimisho hayo Dkt.Mwinyi ametoa Tunzo kwa Mamlaka za Kuzuia Rushwa ZAECA na TAKUKURU kutokana na kazi yao kubwa wanazozifanya za kupambana na Vitendo hivyo
Maadhimisho ya kupambana na Rushwa Afrika kufanyika Tarehe Kumi na Moja Mwezi wa Saba ya Kila Mwaka ambapo Mwaka huu imebeba Ujumbe wa Mifumo Madhubuti ya Ulinzi wa Taarifa, ni nyenzo muhimu katika Mapambano dhidi ya Rushwa.