DKT.MWINYI AZIPONGEZA ZAECA NA TAKUKURU KWA KUOKOA FEDHA NA MIRADI YA MAENDELEO NCHINI

DKT.MWINYI

   Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti Baraza la Mapinduzi Dkt.Hussein Ali Mwinyi amezipongeza  Mamlaka za kuzuia   Rushwa  na Uhujumu   Uchumi Zanzibar na Tanzania ZAECA na  TAKUKURU    kwa kufanikiwa kuokoa Fedha nyingi   na kusimamia Miradi mbali mbali  ya maendeleo Nchini.

    Akizungumza katika Maadhimisho ya Siku ya Mapambano dhidi ya Rushwa Afrika yaliyofanyika katika Ukumbi wa Kimataifa wa Maonenyesho Nyamanzi Dkt.Mwinyi amesema Mapambano dhidi ya Rushwa na Uhujumu Uchumi ni miongoni mwa vipaumbele  vya Serikali katika kuandaa mipango madhubuti itakayosaidia  kuokoa hali ya Uchumi wa Nchi .

    Amesema katika kufanikisha hilo Serikali inameanza kutumia  sheria ya kumlinda mtoa Taarifa za Rushwa na Uhujumu Uchumi dhidi ya mtuhumiwa ambayo hatua hiyo itamsaidia kumpa ulizi na usalama wa Maisha yake

   Mkurugenzi Mkuu wa ZAECA Ali Abdallah Ali  na Naibu Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU Neema Mwakalile wamesema wataendelea kushirikiana kufuatilia vyanzo vya Miradi ya Maendeleo pamoja na Maeneo ya Rushwa ili hali hiyo isiendelee kufanyika.

    Katika Maadhimisho hayo Dkt.Mwinyi  ametoa Tunzo kwa Mamlaka za Kuzuia Rushwa  ZAECA na TAKUKURU kutokana na kazi yao kubwa wanazozifanya za kupambana na Vitendo hivyo

    Maadhimisho ya kupambana na Rushwa Afrika kufanyika Tarehe Kumi na Moja  Mwezi wa Saba ya Kila Mwaka ambapo Mwaka huu imebeba Ujumbe wa Mifumo Madhubuti ya Ulinzi wa Taarifa, ni nyenzo muhimu katika Mapambano dhidi ya Rushwa.

stories
standard
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.