NECTA YATANGAZA MATOKEO YA KIDATO CHA SITA NA UALIMU KWA MWAKA 2024

KATIBU NECTA

   Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA) limetangaza Matokeo ya Kidato cha Sita na Ualimu kwa Mwaka 2024 yanaoonyesha Ufaulu kwa Ujumla umepanda kwa Asilimia Sifuri Nukta Mbili, Sita  ukilinganisha na Mwaka uliopita.

    Akitangaza Matokeo katika Ofisi za Baraza hilo Zanzibar  Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA) Dkt.Said Ali Mohammed  amesema Matokeo hayo yamepanda kwa Masomo yote na Ufaulu wake upo Zaidi ya Asilimia 90.

     Amefahamisha kuwa kwa Mwaka 2024 Watahiniwa wa Skuli Laki Moja na Mbili Mia Saba 19 sawa na Asilimia 99 Nukta 4 wamepata Ufaulu wa Madaraja la Kwanza hadi la Tatu hivyo ubora wa Ufaulu umeongezeka ikilinganishwa na Mwaka 2023.

    Jumla ya Watahiniwa Laki 1 Elfu 13 Mia 536 wamefanya Mtihani wa Kidato cha Sita, Mwaka huu ambapo umefanyika katika  Skuli 931 na Vituo vya Watahiniwa wa Kujitegemea 258.

stories
standard
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.